Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 8:45 am

NEWS: JAJI MKUU APIGA MARUFUKU KWA MAJAJI KUPOKEA AMARI YOYOTE

JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesema ni marufuku kwa Majaji na Mahakimu kupokea amri ama maelekezo ya aina yoyote ya namna ya kuendesha mashauri mahakamani au kufikia maamuzi ya kimahakama katika kesi.

Prof. Juma ametoa Marufuku hiyo Jana Novemba 18, 2019 alipofungua mafunzo ya wiki tatu ya majaji wapya 12 yanayofanyika Kituo cha Mafunzo Kisutu kwa wiki moja, kisha wiki mbili nyingine watamalizia mafunzo Chuo cha Mafunzo Lushoto.

“Wakati wa kazi zenu za ujaji mtakumbana na majaribu mbalimbali ya uhuru wenu, mtaweza kupambana na majaribu hayo iwapo mtabakia kwenye viapo vyenu.

“Msome kanuni zinazotoa mwongozo ambazo zinaelekeza kuwa ofisa wa mahakama Tanzania analindwa na misingi ya usawa, haki na maadili katika kazi zake.

“Kanuni ya kwanza inamtaka kila mmoja kujikinga kuingiliwa kazi, hata kutoka kwa ndugu zenu, marafiki na hata wenzenu.

“Kanuni zinaeleza kuna mazingira ambayo baadhi ya wanafamilia wanaweza kujitokeza na kutoa mwongozo wa namna ya kufanya kazi zenu, kanuni hizi zinawakumbusha msiruhusu wengine kuonyesha wako katika nafasi muhimu ya kuathiri kazi zenu,” alisema.

Alisema kanuni hizi zinazohusu uhuru wa kufanya kazi zinaenda wakati mwingine zikasababisha kujitoa kwenye shauri lililopo mbele yako ili ionekane uko huru.

“Mfano kanuni ya pili inakutaka ujiondoe kwenye shauri pale ambapo uhuru wako unaweza kuhojiwa, kuna maamuzi mbalimbali ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa, mna haki ya kupitia na kuona umuhimu wa kujitoa.

“Mfano kesi ya Mwita Chacha na wenzake iliyoamuliwa mwaka 2007 na Mahakama ya Rufani, unakumbuka jaji anaweza kujitoa pale anapoona anaweza kuegemea upande mmoja katika uamuzi wake, unapaswa kutoa sababu kwanini unajitoa.

“Ofisa wa mahakama hatakiwi kujitoa bila kutoa sababu za msingi, hii inaweza kusababisha ucheleweshaji na mzigo kwa ofisa mwingine atakyepangiwa shauri hilo.

“Utayari wa kujitoa bila sababu za kutosha ni ubakaji wa kazi za kimahakama na utachochea maombi yasiyo ya msingi kwa maofisa wa mahakama kujiondoa katika mashauri mbalimbali pale wanapoombwa na wadaawa kufanya hivyo.