Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:23 am

NEWS: JAGUAR ARUDISHWA MAHABUSU BAAADA YA KUNYIMWA DHAMANA

Mwanamuziki na Mbunge wa jimbo la Starehe, nchini kenya Charles Njagua maarufu Jaguar analazimika kulala tena mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa baada ya leo Mahakama kumnyima dhamana huku Hakimu Sinkiyan Tobiko akisema atatoa hukumu ya kesi hiyo siku ya Ijumaa.

Wakati Hakimu Tobiko akisema hayo, Mwendesha mashtaka wa Serikali ameiomba Mahakama kuwa Jaguar ashikiliwe kwa siki 14 katika Kituo cha Polisi cha Kamukunji ili kuwezesha kumalizika kwa uchunguzi

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kituo cha habari cha Citizen cha Kenya, makaratasi ya Mahamama yanasema hali ya kiintelijenisia inaonesha Jaguar alipanga kuunda kikundi cha Watu na kuvamia Wageni waishio Kenya

Mwendesha Mashtaka amesema kuwa Wapelelezi wamewaandikia Mamlaka ya Mawasiliano na wanafanya taratibu za kuviandikia vyombo vya habari ili kupata video inayomuonesha Jaguar na matamshi yake

Aidha, Wapelelezi wameeleza zaidi kuwa wanashikilia simu ya mkononi ya Mbunge huyo ila bado haijafanyiwa uchunguzi wowote

siku za hivi karibuni Jaguar ambaye ni mwanamziki wa kibao cha 'Kigeugeu ' alitembelea kwenye moja ya sehemu ya jimbo lake la starehe katika soko moja la jijini Nairobi na kutoa kauli kali na yakibaguzi, Kauli ambayo ilisababisha taharuki ya kidiplomasia baina ya nchi za Afrika Mashariki. “Kama utatembelea masoko, Waganda na Watanzania dio waliochukua biashara yote. Sasa tunasema imetosha. Kama wataona muda wa saa 24 wa kuondoka haraka nchini hautoshi, tutawaondoa kwa nguvu na tutawapiga na hatutamuogopa mtu,” alisema Njaguar.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aliliambia Bunge kuwa Serikali imezungumza na Balozi wa Kenya nchini pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Kenya kuhusu kauli hiyo. Alisema kuwa Serikali ya Kenya imeeleza kuwa kauli ya Njagua sio msimamo wa Serikali na kwamba ni kauli yake binafsi.