Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:47 pm

NEWS: JAFO: ''VIONGOZI WANASHINDWA KUSIMAMIA NIDHAMU KWA VILE WAO HAWANA NIDHAMU''

DODOMA: Naibu waziri,ofisi ya Rais ,TAMISEMI Selemani Jafo amewataka viongozi wakuu wa wilaya, Wakurungezi na halmashari kuwa na nidhamu katika utendaji wao wa kazi ili kuleta ushirikiano mzuri katika jamii.

‘’viongozi wanashindwa kusimamia nidhamu kwa kuwa wao hawana nidhamu ‘’ amesema jafo

Ameyasema hayo wakati wa kufungua semina ya mafunzo ya uongozi wa wakurungezi na wakuu wa wilaya toka nyanda za juu kusini Dar es salaam na shinyaga iliyofanyika mjini Dodoma .

Jafo amewataka kuwa na mahusiano mazuri katika utendaji ili kuweza kutekelezailani yachama cha mapinduzi kamaserikali ilivyotoa maelekezo.

‘’ kuna wakati mwingine mkurungezi na wakuu wa wilaya mahusiano ni hafifu mimi naamini baada ya mafunzo haya mtaenda kufanya yaliyo mema’’

Hata hivyo amewataka viongozi kutunza siri za ofisini ili kuweza kusimamisha misingi yautendaji wa kazi

Amesema miongoni mwa mada zitakazo jadiliwa kwenye semina hiyo ni kupambana na madawa ya kulevya, maadili katika kazi.

‘’ Naamini huko mnako kwenda mtaenda na kupambana na madawa ya kulevya na kusimamiauvujaji wa siri katika maeneo yenu’’ amesema jafo

Akifafanua zaidi amesema ili Tanzania kufikia uchumi wa viwanda ni lazima viongozi kusimamia suala la amani na utulivu katika maeneo.

‘’Kama kuna migogoroya mipaka,serikali na wananchi, kama migogoro wafungaji na wakulima kwa kipindi kirefu nchi yetukwa hiyo tukisimamia nchi yetu kwa ubora zaidi malengo ya Tanzania ya viwanda tutaweza kuyatimiza vizuri ’’

‘’Nendeni mkasimamia mapato ya serikali, serikali tumeelekeza katika makusanyo kwa kutumia mfumo wa kieletroni kabla yakuanza kutumia mfunzo huu makusanyo ya mwezi katika halmashauri hospitali za wilaya zilikuwa zinakusanya Tshs bilioni 4 hadi 6 ‘’ amesema

‘’Baada ya kusimamia makusanyo hayo kwa mfumo wa kieekroniki serikali inakusanyatshs bilioni 24 mpaka 60 kwa mwenzi utofauti ni kubwa sana kwahiyo nendeni mkasimamie ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha katika halmashauri’’ Amesema Jafo