- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO: ''NANENANE SIYO SEHEMU YA KUUZIA MABESENI NA NGUO ZA NDANI''
DODOMA: NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), Selemani Jafo amewashukia, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa mikoa ya Dodoma na Singida kwa kushindwa kufanya maandalizi ya uhakika ya Nane nane kanda ya kati.
''Jafo amesema kuwa inasikitisha kuona maonesho ya nanenane yanageuzwa kuwa soko la kuuza nguo za ndani na mabeseni ya kuogea watoto badala ya kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji.''
Jaffo amesema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya wakulima nanenane kanda ya kati yaliyofanyika katika kiwanja cha Nzuguni mjini hapa.
Akifunga madhimisho hayo alisema lengo la kuwepo kwa nane nane ni kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji ili kuwawezesha kutoa elimu bora kwa wakulima kulima kilimo chenye tija badala ya kile cha kijikimu.
Alisema haiwezekani maonesho ya nane nane ambayo yapo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji yakageuzwa kuwa sehemu ya kuuza beseni za kuogeshea watoto pamoja na kuuza nguo za ndani na mitumba.