- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO AWATAKA WAKANDARASI KUZINGATIA MUDA WA MIKATABA.
SIMIYU: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Selemani Jafo amewataka wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia muda uliowekwa katika kukamilisha miradi hiyo.
Jafo aliyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi pamoja na Halmashauri ya Maswa.
Katika ziara hiyo, Jafo alikagua ujenzi wa kituo cha mabasi kipya ya Mji wa Bariadi pamoja na barabara, ujenzi wa viwanda viwili vya Chaki na Vifungashio katika halmashauri ya Maswa, pamoja na ujenzi wa barabara za lami ndani ya Mji wa Maswa zinazojengwa na TARURA.
Jafo amewataka wakandarasi hao wakiwemo SUMAJKT wanaojenga viwanda vya Chaki na Vifungashio kukamilisha kazi zao ndani ya muda waliopewa bila kuleta visingizio mbalimbali.
Jafo amemaliza ziara yake Mkoani Simiyu kwa kuwapongeza viongozi na watendaji wa Mkoa huo kwa mshikamano wao katika kusimamia miradi ya maendeleo.