Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:48 pm

NEWS: JAFO AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUKEMEA MATENDO MAOVU.

DODOMA: Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa dini kwakuwa mstari wa mbele katika kuliombea Taifa na kuwaomba kuendelea na moyo huo na kukemea vitendo viovu.

Jafo ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika semina ya siku tatu ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kikiristo mkoani Dodoma.

Naibu Waziri Jafo amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kusimamia maadili kwa kuendelea kukemea matendo maovu yakiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, rushwa na mauaji ya vikongwe.

Aidha Jafo amewaomba viongozi hao wa dini kupinga mambo yote yasiyo mpendeza mungu.

Akizuzungumzia kuhusu amani na utulivu hapa nchini, Jafo amesema kwasasa nchi inapoelekea katika uchumi wa viwanda ni vyema viongozi hao wakaendelea kuliombea Taifa kwa kuwa bila amani malengo hayawezi kufikiwa.

“Nawaomba pia muendelee kumuombea Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayo ifanya kwa manufaa ya wananchi wote,”amesema Jafo