- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO AWAGEUKIA WANASIASA UCHAGUZI SEREKALI ZA MITAA
Dar es Salaam. Waziri ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo amewataka wanasiasa nchini kuwa makini na kauli zao wanazotoa ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kuhitimishwa kwa zoezi la wagombea kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 24, 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Novemba 3, 2019, Jafo amesema uchukuaji wa fomu umekwenda vizuri katika maeneo mengi na zilipotokea dosari aliagiza hatua zichukuliwe kwa haraka.
“Tunapata malalamiko kutokana na dosari za hapa na pale katika maeneo machache na kwa haraka tunatoa maelekezo kwa wasimamizi na watendaji, kuruhusu mchakato huo kufanyika bila usumbufu,”
“Niwaombe wana siasa kuacha kutoa kauli tata lengo ni moja kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu. Pia nivisihi vyama visicheze rafu huko maana kuna malalamiko mengine yanakuja upinzani kwa upinzani wanahujumiana,”
Kumekuwepo na malalamiko kutoka vyama vya upinzani nchini vikilalamikia misukosuko wanayopata wangombea wa vyama vya hivyo kote nchini juu ya vitendo vinavyofanywa na watendaji wa kata.
Chama kikuu cha upinzani chadema kimelalaka na kumuandikia barua Waziri Jafo juu ya hujuma na njama wanazofanyiwa na watendaji hao.
Chama kingine ni ACT Wazalendo nao pia wameonesha dosara kwenye maeneo mengi kwenye kipindi hiki cha wagombea kuchukua fomu.