- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO ATOA SOMO KAMPENI YA ONDOA 'ZERO' KISARAWE.
DAR ES SALAAM: MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kuanza mchakato wa kuwaweka wanafunzi wa kidato cha nne katika kambi maalum ya masomo kwa ajili ya kujiandaa na mitihani.
Kambi hizo zinatakiwa kuwekwa katika shule zao kuanzia Oktoba mosi mwaka huu hadi pale watakapomaliza mitihani yao ya kidato cha nne mnamo Novemba 19, 2017.
Jafo ameazimia Kampeni hiyo leo alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe ya mahafari ya kidato cha nne katika sekondari ya Maneromango iliyopo wilayani kisarawe.
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kupata muda wa kutosha kujisomea ili kuondoa tatizo la ufaulu usio ridhisha jimboni humo.
Naibu Waziri Jafo ameipa Kampeni hiyo jina la Ondoa ZERO Kisarawe ambapo itagusa shule zote za kata zilizomo wilayani humo ambapo wanafunzi watakula na kulala, na kufanya mazoezi mbalimbali ya masomo ili kuwajengea uwezo wanafunzi hao kabla ya kuanza mitihani yao.
Katika kufanikisha zoezi hilo, Jafo amewaagiza viongozi wote wa wilaya ya Kisarawe kuandaa harambee maalum kwa kuwashirikisha ya wadau mbalimbali wa maendeleo wa Kisarawe.
kampeni hiyo inahitaji wastani wa shilingi milioni 50 kwa ajili ya wanafunzi 669 wa kidato cha nne watakaokuwa kambini.
Kadhalika, Harambee maalum ya wadau inatarajiwa kufanyika Oktoba 7, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Jafo amewapongeza viongozi wote wa kisarawe pamoja na wananchi wa Maneromango kwa kufanikisha ujenzi wa mabweni mapya mawili, maktaba, madarasa, pamoja na matundu ya vyoo kumi shule hapo baada ya serikali kupeleka kiasi cha shilingi milioni 259.