- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO ATEMA POVU KWA WADAU WA MAENDELEO
DAR ES SALAAM: Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewapongeza wadau mbalimbali nchini kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Jafo ameyasema hayo alipokuwa akizindua Mpango mkakati asasi ya watathimini nchini uitwao Tanzania Evaluation Association (TanEA) uliofanyika Julius Nyerere Conference Centre jiji Dar es salaam.
Taasisi hiyo imefanikiwa kuzindua mpango mkakati huo wa miaka mitano kuanzia 2017 - 2021 ambao unalenga kufanya tathmini ya mipango mbalimbali ya maendeleo nchini ili kuweza kutoa mwanga kwa maeneo yaliyo fanyika vizuri na maeneo ambayo hayakupata mafanikio yaliyo kusudiwa ili kuiwezesha Tanzania kutimiza dhamira ya kufikia nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia uchumi wa viwanda.
Akizungumza katika uzinduzi huo Jafo amezitaka taasisi mbalimbali hapa chini pamoja na taasisi za kimataifa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo hapa nchini.