- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO ATAKA JENGO LA AKINA MAMA KUKABIDHIWA 20 OKTOBA.
DODOMA: NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo ameuangiza uongozi wa hospital ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma ifikapo oktoba 20 mwaka huu jengo la wodi ya kinamama liwe limekamilika.
Jafo amesema lengo la kukamilika kwa wodi hiyo ni kuharakisha huduma ya matibabu kwa wananchi hususani akima mama na watoto na huduma hiyo itasaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Mbali na hilo amesema kuwa hospitali ya rufaa ya Dodoma ni kati ya hospitali muhimu kutokana na Dodoma kuwa makao makuu hivyo imekuwa ikipokea wagomjwa wengi wakiwemo viongozi mbalimbali wa kiserikali na wa kisiasa.
Ameyasema hayo jana alipofanya ziara yake ya kawaida ya kikazi katika hospital hiyo mkoani hapa.
‘’Dhumuni kubwa la kutembelea hospitali hii ni kwa sababu tuna fahamu wazi Serikali imehamia rasimi Dodoma kwahiyo tunakila sababu ya kuimarisha sekta ya afya na mambo mengi ‘’ alisema .
‘’Kwahiyo nimekuja kuangalia hali halisi hasa ya kimiundombinu yautoaji wa afya ikoje lakini kipindi cha nyuma wakati tunazindua jengo la bima ya afya tulikuwa na bajeti yetu ya mwaka wa fedha kwahiyo nimekuja kujiridhisha fedha hizo zimetumikaje lakini nimefarijika ujenzi unaendelea vizuri ’’ amesema
Katika hatua nyingine Jafo ameuagiza uongozi wa hospitali ya mkoa pamoja na mkandarasi kuhakikisha wanafunga mfumo wa usambazaji wa hewa ya Oksijen katika wodi ya akina mama ili kuondokana na tabia ya kubebelea mtungu wa hewa ya oxgen pale mgonjwa anapohihitaji.
Pia Jafo aliangiza uongozi huo kufanya tathimini ya haraka nini kifanyike ili jengo hilo liweze kukamilika.
Aidha ameuagiza uongozi wa hospitali ya Mkoa kuhakikisha wanafanya ukarabati wa majengo yote huku akisema kuwa pale ambapo wanatakiwa kufanya ujenzi ni vyema wakajenga majengo ya juu(Ghorofa ) badala ya kuendelea na ujenzi wa majengo mafupi ili kuweza kupata nafasi.
Amesema ili kufanya ukarabati wa majengo hayo serikali itawezesha kutoa kiasi cha sh.milioni 500 ili kufanikisha jambo hilo ili hospitali ya mkoa iweze kuwa na hadhi ambayo inastahili.
Hata hivyo alisema kutokana na humuhimu wa Dodoma kuwa makao makuu kuna kila sabau ya kufanya ukarabati na upanuzi wa chumba cha upasuaji ambacho kinaonekana kuwa na changamoto kubwa licha ya kuwepo na madaktari bingwa katika hospitali hiyo.
Kwa upande wake mganga kuu wa hospitali hiyo Dk. Charles Kiologwe alisema changamoto kubwa katika hospitali hiyo ni kukwama kiutendaji
‘’ Changamoto ni kubwa ni Kuna kukwama kiutendaji ila kuna changamoto zinazojitokeza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma inapokea wagonjwa 400 mpaka 800 kwa siku lakin hospital hii miaka mingi kidogo mwaka 1929 na uchache wa maeneo ‘’ alisema
Mradi wa ujenzi wa wodi ya kina mama unafadhiliwa na kampuni ya PAMCON interconstruction limited ulianza mwaka 2011 mpaka sasa ni miaka sita.