- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO ASEMA MKURUGEZI ALIYEMPIGA MTU RISASI ALIFANYA KWA UTASHI WAKE
Singida: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amelaani vikali vitendo cha watumishi wa umma kutumia nguvu nyingi dhidi ya wananchi hali inayopelekea kuletea machafu kwenye jamii na hata kupelekea mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia.
Jafo amelaani vitendo hivyo wakati wa mazishi ya marehemu Isaka Petro aliyefariki jumamosi baada ya kupigwa risasi na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Itigi katika vurugu zilizotokea katika kanisa la Waadiventisti Wasabato Itigi kundi Namba Two na kuzikwa nyumbani kwao kijiji cha kazikazi kata ya Kitaraka; Mazishi hayo pia yamehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Singida pamoja na Wilaya ya Manyoni.
Jafo amesema tukio hilo lilitokea sio agizo la Serikali na waliotekeleza wamefanya kwa utashi na akili zao binafsi na hawakuagizwa na mtu yeyote na zaidi wametenda kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.
“Hakuna namna tunaweza kusema vinginenevyo kuhusu tukio hili zaidi ya kuwa tukio baya na la kusikitisha sana kuwahi kutokea kwa wananchi wetu, tena likiwa limetekelezwa na watumishi wa Serikali inasikitisha sana nawasihi watumishi wa umma tutangulize utu mbele katika kila kazi tunazozifanya”
Aliongeza kuwa watumishi wa umma haijalishi unafanya kazi gani katika mazingira gani lakini hakikisha unatanguliza ubinadamu kwanza ili tulinde maisha yetu na ya wale tunaowahudumia haipendezi wewe ukawa chanzo cha mtafaruku katika jamii tusaidie kuwaunganisha wananchi na kuwafanya kuwa kitu kimoja na sio kuwa chanzo cha ugomvi na mafarakano.
Kwa taarifa nilizopewa na nimezithibitisha ni kuwa wote waliohusika na tukio hili wameshakamatwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama bado vinaendelea na taratibu zao alisema Jafo.
Katika msiba huo Waziri Jafo akiwa na viongozi wa Mkoa wa Singida alitoa pole kwa familia ya marehemu sambamba na rambirambi pia alishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki katika shughuli zote za mazishi ya marehemu Isaka Petro nyumbani kwao kazikazi.
Akizungumza katika mazishi hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa msimba huo ni pigo kwa Serikali pamoja na wananchi wote wa kijiji cha kazikazi.
“Serikali inawahudumia wananchi walio hai na sio wafu sasa mwananchi wetu anapotutoka tena kwa kifo cha kwa namna hii na sisi tunapata pigo kwa sababu dhamira yetu ya kufikisha huduma bora kwake haitafikiwa”
Sisi kama Serikali tuna wajibu wa kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya wananchi wetu kufanya shughuli zao kwa usalama wa hali ya juu sasa wajibu huu unapotekelezwa kinyume na taratibu zetu ni makosa ninatoa na kila mtu atawajibika kwa kadiri ya kosa lake alisema Dkt. Nchimbi.
Aidha Dr Nchimbi aliwaeleza wananchi wa kazikazi pamoja na Kitaraka kuwa wale wote wanaolima katika Shamba la Kitaraka waendelee na shughuli zao kama kawaida na wasilipe ushuru wa shilingi elfu ishirini kama ilivyokuwa hapo awali mpaka hapo yatakapokuja maelekezo mengine.
“Watumishi wa halmashauri mupeleke ujuzi na pembejeo kwa wakulima wadogo wa shamba la Kitaraka na sio kwenda kuwabugudhi kwa kuwadai ushuru nyie endeleeni na wawekezaji wenu wakubwa kwa kadiri ya makubalino mliyoingia lakini hawa wananchi wanaolima ekari moja moja waacheni waendelee na kilimo chao” alisema Dkt. Nchimbi.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato Itigi Kundi Namba Two Manigina F.S Manigina aliwaasa wanakijiji cha kazikazi kutokua na kisasi na kumuomba Mungu ili tukio kama hilo lisitokee tena katika kijiji chao.
“Visasi ni vya Mungu nyinyi msiweke visasi na mtu ila endeleeni na maisha yenu kama kawaida na Mungu atazidi kuwashushia baraka zake katika kazi zenu” alisema Mchungaji Manigina.
Katika vurugu zilizotokea siku ya jumamosi katika kijiji cha kazikazi eneo la Kanisa la Waadiventista Wasabato Kundi Namba Two baina ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi akiwa na askari wa wanyamapori na baadhi wa wananchi wa kijiji hicho zilipelekea kifo cha kijana Isaka Petro mwenye umri wa miaka 28.
Marehemu ameacha mke na watoto watatu.