- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI MEDELI.
DODOMA: Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selamani Jafo amewataka Watanzania kupanda miti katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha lengo ikiwa ni Kurejesha hali ya asili ya mazingira iliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu na kuongeza kuwa upandaji miti ni kuweka mazingira safi.
Akizungumza leo Jijini Dodoma katika zoezi la upandaji miti maeneo ya medeli kata ya Tambuka reli Wilaya ya Dodoma mjini amesema kuwa lazima watanzania watumie njia hizo ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa yakijani nakuwataka wanafunzi ambao hawajapanda mti watekeleze zoezi hilo.
Aidha,waziri Jafo amesema ajenda ya mazingira ndiyo ajenda inayosababisha uchumi kuwa imara huku akiwataka wanafunzi kupeleka ujumbe kwa wazazi wao kushiriki katika zoezi zima la kupanda Miti katika maeneo yao.
Serikali imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha inatunza mazingira ili kuwa na mazingira safi miongooni mwa mikakati hiyo ni upandaji miti katika taasisi za serikali na binafsi nchini.