- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFO AMTAKA MENEJA WA TARURA KUHAKIKISHA BARABARA ZINAZOJENGWA ZIWE NA UBORA.
MOROGORO: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amemtaka meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini(TARURA) Manispaa ya Morogoro kuhakikisha barabara za lami zinazojengwa ndani ya manispaa hiyo zinakuwa katika ubora unaotakiwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi wa barabara hizo huku akibaini kuharibika kwa baadhi ya barabara za lami zilizojengwa miaka michache iliyopita.
Amesema kuwa ujenzi wa barabara za lami umekuwa ukitumia gharama kubwa hivyo ni vyema Meneja huyo akahakikisha anasimamia ili ujenzi wake uwe kwenye viwango vinavyotakiwa.
“Haiwezekani tunatumia fedha nyingi lakini barabara zinaharibika ndani ya muda mfupi wakati wahandisi mnaosimamia mpo.Sitamvumilia mhandisi yeyote kwa miradi inayojengwa endapo haitakidhi viwango,”amesema Jafo.
Jafo amewaonya mameneja ya TARURA wa wilaya ambao watashindwa kusimamia kazi zao ipasavyo katika halmashauri zao wanazozisimamia kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua.