Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:25 am

NEWS: JAFO AITAKA JAMII KUWAHESHIMU WAZEE

ILI kufikia uchumi Wa kati na viwanda nchini jamii imetakiwa kulinda na kuthamini mchango Wa wazee katika kukuza uchumi Wa taifa letu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wa Tamisemi Selemani Jafo wakati akizindua maadhimisho ya Siku ya wazee duniani ambayo yalifanyika Jana mjini hapa.

" Tuwaenzi wazee wetu kwa busara tuseme wahenga wetu katika mitandao ya kijamii kwa mazuri waliyoyafanya kwa kupigania Uhuru wetu na kuli fikisha taifa hapa lilipo"alisema.

Jafo aliwagiza wakuu wa wilaya na mikoa nchi zima kuhakikisha wanatoa vitambulisho vizuri na kuweka mikakati ili kuepusha usumbufu unaoendelea kujitokeza kwa wazee hao.

Pia aliwaangiza watendaji wa serikali kufanya kambi maalumu za kupima afya kwa wazee kwa kila mkoa ili kuondokana na uzalilishaji wanaopata wazee pindi wanapohitaji huduma ya afya.

‘’Wakuu wa wilaya na mikoa nawaagiza kuwachukulia hatua kali watakaobainika kuwatendea vitendo vya kikatili na kuwanyanyasa wazee’’alisema Jafo.

Katika maadhimisho hayo wazee zaidi ya wazee 100 walipima afya zao.

Maadhimisho hayo hufanyika mosi oktoba kila mwaka ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema kueleza uchumi wa viwanda,uthamini mchango, uzoefu na ushiriki wa wazeekwa maendeleo ya Taifa ikiwa inahimiza serikali ,jamii na wadau wote wa maendeleo kuona umuhimu wa kushirikisha wazee ili kutumia uzoefu walionao kufikia maelengo ya taifa ya kujenga uchumi na maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.