- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: JAFFO ATISHIA KUZINYANGANYA HALIMASHAURI ZOTE PESA ZA UJENZI
Dodoma: Naibu waziri wa nchi ofisi ya rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Seleman Jaffo ametoa muda wa mwezi mmoja na nusu kwa halmashauri ambazo hazijaanza ujenzi wa ofisi zao licha ya serikali kutoa fedha kwa ajili wa ujenzi huo zitanyang”anywa fedha hizo na kupewa hamashauri nyingine.
Hata hivyo Jaffo ametembelea katika eneo la ujenzi wa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya chamwino katika manispaa ya Dodoma na kuridhika na hatua ya ujenzi wa ofisi hiyo huku akitoa onyo kwa baadhi ya halmashauri ambazo hazijaanza ujenzi wa ofisi zao.
Mradi huu wa ujenzi unajengwa na SUMA JKT ambao wameahidi kukamilisha sehemu ya chini ya jengo hilo ndani ya miezi minne.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino Athuman Masasi amesema kukamilika wa ofisi hizo itasaidia ufanisi wa kazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo.
Naibu Jaffo ameagiza kukamilika mapema kwa ujenzi huo na kuanza kutumika kwa ofisi hizo kuanzia january mosi mwaka 2018, huku Ujenzi huo ukigharimu zaidi ya shilingi milion miasaba kwa sehemu ya chini ya jengo hilo.