Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:55 pm

NEWS: ISRAEL YAFANYA MASHAMBULIZI UKANDA WA GAZA LEO

Jeshi la Israeli limefanya mashambulizi usiku mzima dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Hamas katika Ukanda wa Gaza na kupeleka askari wa ziada kwenye mpaka na Palestina.

media

Hatua hiyo imechukuliwa saa chache tu baada ya shambulio la roketi moja iliyojeruhi watu saba karibu na mji wa Tel Aviv.

Jumatatu jioni, Hamas na makundi kadhaa yanayobebelea silaha katika Ukanda wa Gaza walitangaza katika taarifa kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yalifikiwa chini ya usuluhishi wa Misri, wakati ndege za Israeli zimeendelea usiku kucha na mashambulizi.

Hakuna taarifa yoyote kutoka serikali ya Israeli kuhusu makubaliano hayo ya kusitisha mapigano.

Tahadhari ilitolewa Jumatatu usiku kusini mwa Israeli, na kuwataka wakaazi kusalia makwao.

Katika Ukanda wa Gaza, Wapalestina wameripoti kwamba ndege za Israeli zimeshambulia maeneo mawili.

Mapigano hayo yalizuka upya Jumatatu asubuhi kufuatia shambulio la roketi iliyorushwa kutoka Ukanada wa Gaza na kujeruhi Waisraeli saba, ikiwa ni pamoja na watoto, kwa mujibu wa mamlaka nchini Israeli.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema kuwa Wapalestina watano wamejeruhiwa katika mashambulio hayo ya angani ya jeshi la Israeli (Tsahal) kwa kulipiza kisasi.

Milipuko ya mabomu imesikika katika maeneo kadhaa ya Palestina, maeneo ambayo wakaazi wengi wametoroka.

Moja ya mashambulio hayo imelenga ofisi ya kiongozi wa Hamas katika eneo la pwani, Ismail Haniyeh, radio ya Hamas imebaini, huku ikiongeza kuwa kiongozi hakuepo wakati wa shambulio hilo. Jumatatu mchana, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambaye anawania muhala mpya katika uchaguzi wa Wabunge wa Aprili 9, aliahidi kulipiza kisasi baada ya shambulio hilo la roketi kutoka Palestina.

Aliamua kufupisha ziara aliyoanza Jumapili nchini Marekani.

Hali si shwani kwenye mpaka kati ya Ukanda wa Gaza na Israeli tangu kuanza kwa maandamano ya haki ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa Palestina wa mwaka 1948 na vizazi vyao nchini Israeli mwaka jana.

Wapalestina wataadhimisha mwaka mmoja tangu kuanza kwa maandamano hayo mwishoni mwa wiki hii.

Takribani Wapalestina 200 wameuawa na majeshi ya Israeli tangu kuanza kwa maandamano hayo Machi 30, 2018.