Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 8:55 am

NEWS: IRAN YAKANUSHA KUIZUIA MELI YA MAFUTA YA UINGEREZA

Jeshi la Iran lilikana kuwa limeizuwia meli ya mafuta ya Uingereza katika mlango bahari wa Hormuz.

Jeshi la kimapinduzi ya Iran limesema katika taarifa kuwa hakukuwa na makabiliano katika muda wa masaa 24 na meli yoyote ya kigeni, ikiwa ni pamoja na meli za Uingereza.

Related image

Serikali ya Uingereza imesema leo kuwa meli tatu za Iran zilijaribu kuzuwia njia ya meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la maji la Ghuba, na kulazimisha meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose kuingilia kati.

"Hakujatokea makabiliano yoyote ndani ya masaa 24 yaliyopita kati yetu na meli yoyote ya kigeni, zikiwemo za Uingereza." Ilisema taarifa fupi iliyotolewa na kikosi hicho.

Mkasa huu unachochea zaidi uhasama unaoendelea kwenye eneo hilo la Ghuba, ambalo tayari liko kwenye hatihati kutokana na mkwamo baina ya utawala wa Rais Trump wa Marekani na Iran juu ya mpango wa nyuklia wa taifa hilo la Kiislamu.

Siku ya Jumatano (11 Julai), Rais Hassan Rouhani aliionya Uingereza kw

Image result for iran block england ship

amba itakumbwa na matokeo mabaya ambayo hakuyataja, kufuatia hatua ya nchi hiyo kuikamata meli ya mafuta ya Iran kwenye eneo la Gibraltar.

Maafisa kwenye eneo hilo, ambalo linamilikiwa na Uingereza licha ya kuwa kwake Uhispania, walidai kuwa meli hiyo ilikuwa ikielekea Syria, ambayo imewekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya, huku Marekani nayo ikiwa na vikwazo vyake dhidi ya mafuta ya Iran.

Iran ilikilaani kitendo hicho inachosema ni haramu, huku Uingereza ikikanusha madai ya maafisa ya Gibraltar kuwa imeishikilia meli hiyo kwa maagizo ya Marekani.

Mkuu wa majeshi ya Ufaransa Francois Lecointre amesema leo baada ya Uingereza kuishutumu Iran kuzisumbua meli za mafuta za nchi hiyo kuwa, hali ya wasi wasi katika eneo la Ghuba haielekei kufikia kiwango cha kutoweza kudhibitiwa.

Lecointre amesema hata hivyo kuna hali ya kupimana nguvu kati ya Marekani na Iran, ambayo inaweza wakati wowote kufikia hatua ya kutoweza kudhibitika.