- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IRAN YAIONYA MAREKANI KUSUDIO LA KUIZUIA MELI YAKE YA MAFUTA
Serekali ya Iran imesema leo Agosti 18, 2019 kuwa imeionya Marekani dhidi ya jaribio la kuikamata meli ya mafuta ya Iran Greece 1 ambayo imeondoka eneo la Gibraltar, licha ya juhudi za Marekani kuizuia kushindikana.
Msemaji wa wizara ya masuala ya nje ya Iran, Abbas Mousavi, amewaambia wanahabari kuwa Iran imetoa onyo kali linalohitajika kwa maafisa wakuu wa Marekani kupitia mifumo yake rasmi kutochukuwa hatua hiyo, maana itakuwa na athari mbaya.
Meli hiyo iliyobadilishwa jina hivi sasa na kuitwa Adria Darya nambari moja badala ya Greece nambari moja imeng'owa nanga Gibralter saa tano za usiku jana. Ratiba ya safari inaonyesha meli hiyo inaelekea Kalamata nchini Ugiriki . Inatarajiwa kuwasili huko jumaapili inayokuja. Balozi wa Iran nchini Uingereza Hamid Baeidinejad amethibitisha kupitia mtandao wa instagram mapema kwamba meli hiyo "imeshaondoka Gibralter baada ya kuzuwiliwa kwa siku 45."
Iran ilikuwa na mzozo wa bahari kuu na Uingereza, tangu jeshi la mshirika huyo wa Marekani kuizuia meli hiyo katika pwani ya Gibraltar, mnamo Julai 4 ikidai ilikuwa inasafarisha mafuta kupeleka nchini Syria na hivyo kukiuka vikwazo vya Umoja wa Ulaya. Wiki mbili baadaye, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran kiliikamata meli ya Uingereza katika eneo la Ghuba katika kile Uingereza ilichokitaja kuwa hatua ya kulipiza kisasi. Hata hivyo, hii leo wizara ya mambo ya nje ya Iran imetupilia mbali dhana hiyo kwamba kulikuwa na uhusiano kati ya visa hivyo viwili vya kuzuiliwa kwa meli.
Viongozi wa Ugiriki hawakusema chochote kuhusiana na mvutano huo. Akiulizwa kama Marekani inaweza kutoa tena maombi ili meli hiyo ikamatwe, msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Iran. Abbas Mousavi amesema tunanukuu:"Hatua kama hiyo na pia mjadala kuhusu suala hilo yatahatarisha usalama wa safari za meli baharini. Akizungumza kupitia televisheni ya taifa, Musavi amesema Iran imetuma onyo kupitia njia rasmi na hasa kwa ubalozi wa Uswisi, na maafisa wa Marekani wasifanye makosa kama hayo kwasababau anasema "matokeo yake yatakuwa mabaya."