- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IRAN YAENDELEA NA VITISHO VIKALI VYA KULIPIZA KISASI DHIDI YA MAREKANI
Taifa la Iran limeendelea kutoa ahadi ya kulipiza kisasi dhidi Marekani ambayo ilitekeleza shambulizi la anga lililomuua kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la nchi hiyo Qassem Soleimani.
Akitoa matamshi sawa na yaliyotolewa na viongozi wakuu wa Iran, balozi wa Iran kwenye Umoja wa mataifa amesema kifo cha Jenerali Soleimani ni sawa na kuanzisha vita na "jibu la hatua ya kijeshi hutolewa kwa njia za kijeshi".
Balozi Majid Takht Ravanchi amekiambia kituo cha televisheni cha CNN kuwa kuuliwa kwa kamanda huyo wa jeshi, Marekani imeingia kwenye awamu nyingine ya vita baada ya kuanzisha ´vita ya kiuchumi´ kwa kuiwekea Iran vikwazo vikali mwaka 2018.
Ravanchi amesema Iran itachukua hatua kali za kulipa kisasi na kwamba nchi yake tayari imeliarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa Tehran inayo haki ya kujilinda chini ya sheria ya kimataifa.
Katika barua yake kwa baraza hilo na kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ravanchi amesema mauaji ya Soleimani ni mfano wa wazi wa ugaidi na kitendo cha kihalifu kinachokiuka kwa kiwango cha juu misingi ya sheria ya kimataifa hususan mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo, viongozi wa mataifa mbalimbali wameonya jana kuwa shambulizi la Marekani lililomua kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran limeongeza kitisho duniani na linaweza kuitumbukiza mashariki ya kati kwenye mzozo mkubwa wa kijeshi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kila upande kujizua dhidi ya kuongeza msuguano akisema
ulimwengu hauko tayari kwa vita nyingine kwenye eneo la Ghuba.
Wito kama huo umetolewa pia na Urusi, Ujerumani, Ufaransa, Muungano wa Falme za Kiarabu, Syria na Saudia Arabia.
Hata hivyo Uingereza, Ujerumani na Canada ambazo ni washirka wa Marekani wamesema Iran inabeba jukumu kwa kile kilichotokea kutokana na tabia yake ya hivi karibuni ya uchokozi wa kijeshi
Katika hatua nyingine bei ya mafuta duniani imepanda jana Ijumaa baada ya Marekani kumuua kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran, kisa kilichozusha hofu ya kuibuka mzozo kwenye kanda ya mashariki ya kati iliyo tajiri kwa mafuta.
Kufuatia kifo cha Jenerali Qasem Soleimani, bei za mafuta zimepanda kwa zaidi ya asilimia 3 kwenye soko la dunia wakati Iran ikionya kuchukua hatua nzito kulipa kisasi dhidi ya Marekani.