- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : INJINI YA NDEGE YAHARIBIKA IKIWA ANGANI NA ABIRIA 500
Abiria 500 wamenusurika kifo baada ya injini moja ya ndege ya abiria ya shirika la Air France kuharibika ikiwa angani.
Ndege hiyo ikiwa imetua nchini Canada kwa dharula.
Ndege hiyo aina ya Airbus 380 (superjumbo) ilikuwa njiani kuelekea Los Angeles nchini Marekani ikitokea Paris, Ufaransa ikiwa na zaidi ya abiria 500.
Ndege hiyo iliamua kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Goose Bay, mashariki mwa Canada.
Abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wameeleza kuwa walianza kuona cheche zikitoka kwenye injini na ndipo walipoanza kutoa taarifa kwa wahusika.
“Tulianza kuona cheche kwenye injini kitu ambacho sio cha kawaida kwani zilikuwa zinaongezeka kila muda ulivyokuwa unaenda huku ikitoa mlio mkubwa kitu ambacho kilizua taharuki ndani ya ndege.“amesema Sarah Eamigh kwenye mahojiano yake na gazeti la New York Daily News.
Tayari shirika la Air France limethibitisha kutokea kwa hitilafu na hakuna mtu hata mmoja aliyejeruhiwa katika tukio hilo, huku wakieleza chanzo cha tatizo hilo kuwa ni kuharibika kwa feni za injini.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la AFP ndege hiyo ilikuwa na abiria 496 na wafanyakazi 24.