Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:30 pm

NEWS: IMF YATANGAZA KUTOA DOLA BILIONI 50 KUSAIDI NCHI ZENYE CORONA

Shirika la fedha duniani (IMF) limetangaza kutoa dola bilioni 50 kuzisaidia nchi zote zilizoathirika na virusi vya ugonjwa wa corona.

Shirika hilo limetoa onyo kuwa mlipuko wa corona tayari umeathiri ukuaji wa kiuchumi wa dunia kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana .

Hatua za dharura zimeanza baada ya virusi hivyo kusambaa nje ya China na kuzifikia zaidi ya nchi 70.

Wiki hii benki ya dunia imechukua hatua ya kupunguza makali ya matokeo ya virusi hivyo.

Image result for IMF against corona virus

IMF ilisema kuwa inatoa fedha kwa ajili ya kuwasaidia nchi maskini na kipato cha kati ambazo mifumo ya huduma zao za afya iko chini.

Wakati huohuo , ufadhili huo utasaidia kukabiliana na janga la kiuchumi kwa sababu kusambaa kwa virusi hivyo kumepelekea uchumi wa dunia kuyumba zaidi mwaka huu wakati janga hilo la kifedha lilianza kushuka taratibu tangu mwaka 2008.

Image result for corona virus

Lakini mkurugenzi wa IMF Kristalina Georgieva ametoa onyo kuwa si rahisi kujua madhara yatakuwa makubwa kiasi gani: "Ukuaji wa kiuchumi duniani kwa mwaka 2020 utashuka ukilinganisha na mwaka jana".

Vilevile alikwepa kusema kuwa janga hili la kiafya linaweza kusababisha uchumi wa dunia kushuka.