- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IKUNGI WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MIRADI YA MAJI.
IKUNGI: Wananchi wa wilaya ya Ikungi wamemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapatia sh bilioni 1.8 kwa ajili ya kuchimba visima na hivyo kuondokana na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji.
Kiasi hicho cha fedha kimetolewa ili kujenga visima katika vijiji 31.
Akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya aliyekuwa anakagua miradi hiyo ya maji kijiji cha Makiungu, mkazi mmoja Thomas Mkinga amesema kwa sasa wanapata shida ya kufuata maji kutokana na visima vilivyopo kuwa vichache lakini kutokana na fedha hiyo ana imani shida hiyo itapungua.
"Tunaishukuru serikali yetu chini ya Rais Dkt Magufuli kwa kutujali, tunamshukuru na kumpongeza Mkuu wetu wa Wilaya Miraji Mtaturu kwa ufuatiliaji uliopelekea kupatikana kwa fedha hizo ili zitekeleze miradi ya maji hapa wilayani kwetu,"alisema mkazi huyo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu amesema miradi hiyo ya maji imeshaanza utekelezaji kwa kasi kubwa kwenye maeneo mbalimbali wilayani humo.
"Kupata fedha hizi ni jambo moja na usimamizi ni jambo la pili, niwaombe wote wenye dhamana ya kukamilisha miradi hii wafanye kwa uadilifu na uaminifu ili miradi ikamilike kwa wakati na wananchi wapate maji kama Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inavyoelekeza, niseme kabisa sitokuwa na mchezo katika hili, tufanye kazi,"alisisitiza Mtaturu.
Amesema dhamira ya Mheshimiwa Rais ni njema hivyo hakuna budi kila mwenye dhamana katika hilo kuibeba dhamira hiyo kwa vitendo ili miradi itekelezwe kwa vitendo na thamani ya fedha ionekane.
Kampuni ya Targets Borewelles ya Dar-es-salaam imepewa tenda ya kujenga visima 8 kazi ambayo inatakiwa kukamilika ndani ya siku 90.
Lengo la wilaya ni kufikia asilimia 85 ya upatikanaji Maji safi na Salama Vijijini ifikapo 2020 ambapo miradi hiyo ikikamilika itaifikisha wilaya kufikia asilimia 71 kutoka asilimia 41 iliyopo sasa ya upatikanaji wa maji.