- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IFAHAMU VIZURI HISTORIA YA KOBE BRYANT
Kobe Bryant aliyezaliwa Agosti 23, 1978 ameacha mke na watoto wakike watatu, mdogo kabisa akiwa amezaliwa mwezi Juni mwaka jana.
Bryant aliingia uwanjani kwa mara ya kwanza mwaka 1996 akiwa na miaka 18 tu, hakuwa na umaarufu, mwaka 2016 alistaafu akiwa ni moja ya majina makubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa kikapu.
Baada ya miaka 20 ya kuchezea timu ya LA Lakers na kushinda ubingwa wa ligi mara tano, namba za jezi mbilia mbazo alizitumia kwa vipindi viwili tofauti , 24 na nane zilistaafishwa kwa heshima yake. Hakuna mchezaji mwengine yeyote ambaye atapewa kuzivaa.
Kifo chake katika umri wa miaka 41 kimeshtua wengi. Binti yake mkubwa Gianna, 13, ni miongoni mwa watu wanane ambao wamefariki pamoja na nyota huyo baada ya helikopta binafsi ya mchezaji huyo kuanguka jana Jumapili.
Kutokana na ubora wake uwanjani alipewa jina na Black Mamba, nyoka mkali apatikanaye katika maeneo mengi barani Afrika.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) Adam Silver, Bryant si tu ni miongoni mwa wachezaji bora tu kuwahi kutokea bali alishawishi wachezaji wengi zaidi kuingia kwenye mchezo huo ulimwenguni kote.
"Familia ya NBA imefadhaika sana na msiba huu mzito wa Kobe Bryant na binti yake Gianna," amesema Silver.
"Kwa misimu 20, ametuonesha unachoweza kufanikisha pale ambapo kipaji cha hali ya juu kinapochanganyika na ari kubwa ya ushindi. Alikuwa ni moja ya mchezaji wa kiwango cha juu kuwahi kutokea.
"Kubwa zaidi, atakumbukwa kama mchezaji mwenye ushawishi mkubwa ambaye aliwafanya watu kunyanyua mpira wa kikapu na kushindana kwa kadri ya uwezo wao.