- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDARA YA UHAMIAJI YATOA ONYO KWA WAHAMIAJI HARAMU.
DODOMA: IDARA ya uhamiaji mkoa wa Dodoma imesema imeandaa mpango maalum wa kuwafikia wananchi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya kwa lengo la kutoa elimu ya utambuzi wa wahamiaji haramu.
Mbali na hilo Idara hiyo imesema kutokana na Dodoma kuwa makao makuu imeimarisha ulinzi wa misako na ufichuaji kwa watu ambao wanaingia nchi kinyume cha sheria kwa nia ya kujipatia fursa zinazotokana na makao makuu.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Peter Kundy, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika uwanja wa mpira wa Jamhuri mjini hapa.
Kundy amesema kutokana na Dodoma kuwa makao makuu ya nchi zipo changamoto nyingi za watu wengine kutoka nje ya nchi kwa lengo la kutaka kutumia fursa za kujipatia kipato.
Amesema idara hiyo kwa sasa inaendesha misako,katika maeneo ya mikusanyiko ya watu kama vile makanisani,misikitini, masokoni na sehemu za starehe kwa lengo la kuwabaini watu walioingia nchini kinyume na utaratibu.
“Ninachowaomba wananchi wa mkoa wa Dodoma ni kuhakikisha wanatoa taarifa kwenye ofisi za idara ya uhamiaji pale ambapo watakuwa na mashaka na ngeni yoyote.
“Na kuwepo kwa ongezeko la watu katika mkoa wa Dodoma kwa maana ya mkoa huu kuwa makao makuu idara ya uhamiaji imedhamilia kutoa elimu kwa jamii kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya pamoja na kuanzisha misako shirikishi” alisema Kundy.
Idara hiyo imesema Dodoma kuwa makao makuu pamoja na fursa ya kupitiwa kwa bomba la mafuta kutoka Uganda kwende Tanga,Kundy amesema idara hiyo itahakikisha wanaofanya kazi nchini wana vibari maalum na hakuna hatakayeingia nchini kinyume na utaratibu.
Hata hivyo Kundy amesema kutokana na umuhimu wa idara hiyo kwa sasa serikali imekusudia kuongeza watumishi ili kuweza kukithi vigezo vya utendaji kazi katika makao makuu ya nchi.