- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDADI YA WATU WENYE CORONA TANZANIA YAFIKIA 19
Dar es Salaam. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema wagonjwa walioambukizwa Virusi vya corona nchini Tanzania wamefikia 19, baada ya vipimo vya ofisi ya Mkemia mkuu kudhibitisha kuongezeka watu watano siku ya leo Jumatatu Machi 30, 2020.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na waziri huyo leo Jumatatu mchana imesema kuwa wagonjwa hao watano walifanyiwa vipimo katika maabara kuu ya Taifa, “kati ya wagonjwa hawa, watatu ni kutoka Dar es Salaam na wawili kutoka Zanzibar ambao taarifa zao zimetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar.”
“Hivyo sasa jumla ya wagonjwa wa corona ni 19 akiwemo mgonjwa mmoja aliyetolewa taarifa na Waziri wa Afya Zanzibar Machi 28, 2020.”
“mwanaume mwenye miaka 29 Mtanzania alikutana na raia wa kigeni kutoka miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi. Mwanamke mwenye miaka 21 Mtanzania ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa.”
“Mwanaume mwenye umri wa miaka 49 Mtanzania ambaye pia ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa.”
Ummy amesema kuwa wataendelea na kazi ya kufuatilia watu wote wa karibu waliokutana na wagonjwa hao, kuwataka watu kuendelea kuchukua tahadhari ili kujikinga na ugonjwa huo ambao hadi leo saa 7:00 mchana, watu zaidi ya 30,000 wameripotiwa kufariki kwa ugonjwa huo.
kuna Kesi ya mgonjwa wa Coronavirus aliyepatikana Kagera kabla ya hii ya leo amabye alikua dereva wa malori makubwa, ambaye aliingia nchini kupitia mpaka wa kabanga akiwa anaendesha magari kati ya DRC, Burundi na Tanzania.
Wagonjwa wote 13 kasoro mmoja wao walisafiri nje ya nchi katika siku 14 zilizopita kabla ya kuthibitika kuwa na virusi hivyo, na mgonjwa ambaye hakusafiri nje ya nchi alikutana na muathirika anayetoka nje ya nchi.
Wiki iliyopita Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kuwa nchi hiyo ina wagonjwa 12 walioambukizwa ugonjwa wa corona.
Wanane kati ya wagonjwa hao ni raia wa Tanzania na wengine wanne ni raia wa kigeni.
Akihutubia taifa rais Magufuli alisema: ''Tumetishana sana Tanzania kana kwamba hakuna magonjwa yanayouwa watu''
''Nimeanza kuwa na wasiwasi kwamba imefika mahali hata watu wanamsahau mungu kwamba Mungu ndiye mponyaji wa kweli katika maisha yetu, ile tuweze kushinda hili balaa lakini pia tunachukua tahadhari.'' aliongezea kusema.
Aidha Bw. Magufuli alisema kuwa ana matumaini kuwa janga hilo litapita.
''Tuchape kazi, tuendelee kumuomba mungu. Tusitishane, tusiogopeshana. Natoa wito kwa ndugu zangu wanaoandika mitandaoni kwa sababu kila mmoja amekuwa akiandika lake. Mengine wanapeleka kama mzaha. Huu ugonjwa sio wa kufanyiwa mzaha.''