- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: IDADI YA WALIOMBUKIZWA CORONA TANZANIA WAFIKIA 254
Wizara ya Afya nchini Tanzania imetangaza kuwa Maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo yafikia 254, hii ni baada ya wagonjwa wapya 87 kuongezeka. Hii leo.
Akitangaza Maambukizi hayo Leo Aprili 20, 2020 Waziri wa Afya nchini Tanzania Ummy Mwalimu amesema idadi hiyo ya wagonjwa 254 ni pamoja na wagomjwa 16 waliotolewa taarifa na Waziri wa afya Zanzibar.
Wagonjwa hao wapya wa Corona 84 ni kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi kama ifuatavyo;- Dar es salaam -33, Arusha -4, Mbeya-3, Kilimanjaro-3 Pwani -3, Tanga-3, Manyara-2, Tabora -1, Dodoma -3, Ruvuma -2, Moro- 2, Lindi-1, Mara-1, Mwanza -3, Mtwara -1, Kagera-1, Rukwa-2, Zanzibar-16.
Bi Ummy amesema kuwa wagonjwa 80 kati ya 84 wanaendelea vizuri isipokuwa Wagonjwa 4 ndio wapo kwenye chumba cha Uwangalizi Maalum(ICU).
Aidha Wizara imesema kuwa katika maambukizi hayo mapya wagonjwa 3 wamepoteza maisha, wote kutoka jijini Dar ea salaam.