Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:24 pm

NEWS: HUYU NDIYE OMARI AL BASHIRU

Rais wa Sudani aliyepinduliwa na jeshi Alhamisi wiki hii, Omar al Bashir alizaliwa mwaka 1944 katika familia ya wakulima kaskazini mwa Sudan, ambayo pia ni sehemu ya ukoo wa ufalme wa Misri.

Alijiunga na jeshi la Misri akiwa kijana mdogo na kupanda ngazi ya uongozi wa jeshi hilo, katika vita dhidi ya Israel mwaka 1973.

Aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka mnamo mwaka 1989 na alichukua madaraka wakati Sudan ilikuwa ikikabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini kabla haijagawanyika (Sudani na Sudani Kusini).

Lengo lake lilikuwa la kuunganisha Sudan, lakini kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu kujitenga kwa Sudan Kusini ilifikiwa kama sehemu ya mkataba wa amani, na hivyo ndoto yake kuzima. Hata hivyo licha ya kutofikia ndoto yake ya kuunganisha Sudan alipongezwa kwa kukubali bila upinzani wowote eneo la Kusini kuwa taifa huru na hivyo kuitwa Sudani Kusini.



Japo alikubali kujitenga kwa Sudani Kusini, aliendelea kulitazama kwa jicho la ajabu jimbo la Darfur - ambalo lilikumbwa na machafuko kuanzia mwaka 2003.



Omar al-Bashiri alishtumiwa na jamii ya kimataifa kuuunga mkono wanamgambo wa kundi la Janjaweed linalotuhumiwa kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya jamii ya Waafrika weusi katika eneo hilo.



Tuhuma zinazomkabili Omar al-Bashiri



Mauaji ya kimbari
Kuwaua watu wa jamii ya Fur, Masalit na Zaghawa
Kuwasababishia mafadhaiko makubwa ya kimwili na kiakili
Kuwaweka katika hali ngumu kwa kuwaharibia makaazi yao


Uhalifu dhidi ya binadamu

Mauaji
Kumpoteza mtu
Kuwahamisha watu kwa nguvu
Ubakaji
Mateso