Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 4:25 pm

NEWS: HUYU NDIYE ALIYEMTOA LISSU MAHAKAMANI

DODOMA: RAIS wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS), TUNDU LISSU ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki,jana aligoma kutoka ndani ya Mahakama ya Wilaya ya Dodoma kwa saa 2 baada ya kupata taarifa kuwa anatakiwa kukamatwa na Polisi kupelekwa Dar es salaam kutokana na kauli zake anaozitoa kudaiwa kuwa ni za kichochezi.

Pia LISSU Aliondoka Mahakamani hapo baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, LAZARO MAMBOSASA kufika Mahakamani hapo na kumtaka kuondoka mahakamani hapo kwani jeshi la polisi halina mpango wa kumkamata.

Tukio hilo limetokea july 19 mwaka huu mahakamani hapo mara baada ya kuahirishwa kesi ya Chama cha Walimu Manispaa ya Dodoma(CWT) iliyokuwa inahusu mgogoro wa viongozi wa chama hicho ambapo LISSU alikuwa akiwatetea viongozi wapya wa CWT wanaodaiwa kufanya matumizi mabaya ya mali za Chama hicho.

Baada ya kuahirishwa kesi hiyo Lissu amesema amepata taarifa za kutaka kukamatwa kupitia ujumbe mfupi kuwa kuna askari waliovalia kiraia wa Dodoma wametumwa kufika Mahakamani hapo ili kumkamata.

MBUNGE huyo alipoulizwa kuhusu chanzo cha kukamatwa kwake, Lissu amesema alitoa kauli hivi karibuni juu ya Rais John Magufuli kuhusu utendaji wake kuwa ni wa kidikteta.

Pia amesema vitisho hivyo haviwatishi wataendelea kusema na kuikosoa serikali hadi watakapofikwa na mauti.

Kwa upande wake, Kamanda Mambosasa alimtaka Lissu kutokimbia kivuli chake na kwamba waliomwambia kwamba askari wanamsubiri ili wamkamate wamemchanganya.

Hata hivyo baada haya kauli hiyo ya kamanda wa polisi LISSU aliweza kuondoka mahakamani hapo na kuendelea na shughuli zake.