- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HUKUMU YA KUMUONDOA PROF. LIPUMBA YAHAIRISHWA HADI MARCH 18, 2019
Dar es Salaam: Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeshindwa kutoa hukumu ya Kesi namba 23 ya mwaka 2016 iliyofunguliwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama chama cha wananchi CUF dhidi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na viongozi wengine 10 wanaomuunga mkono Prof Lipumba, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, ambaye pia ni mbunge wa Kaliua Tabora, Madgalena Sakaya. Wanaiomba mahakama hiyo itoe amri ya kubatilisha barua ya Msajili inayomtambua Profesa Lipumba kuwa ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, wakidai kuwa hana mamlaka na imzuie kuingilia masuala ya ndani ya kiutawala ya chama hicho.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka Machi 17, 2019 ingawa tarehe hiyo iliyopangwa siyo siku ya kazi na badala yake itakuwa siku inayofuata March 18,2019
Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa leo Ijumaa, Februari 22, 2019 na Jaji Benhajj Masoud aliyekuwa akiisikiliza kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho. Hukumu hiyo imeahirishwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Sharmillah Sarwatt.
Akiahirisha hukumu hiyo Naibu Msajili, Sarwatt amesema Jaji Masoud ambaye alitarajiwa kuisoma anakabiliwa na majukumu mengine. “Hivyo nina ahirisha usomaji wa hukumu hii hadi Machi 17 mwaka huu,” amesema Naibu Msajili Sarwatt akitaja tarehe hiyo baada ya kuwasilishwa na karani wa Jaji Masoud.
Hata hivyo, tarehe hiyo itakuwa ni siku ya Jumapili siku ambayo huwa hakuna shughuli za kimahakama.
Profesa Lipumba ambaye Agosti 5, 2015 aliandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo, Juni 5, 2016 aliandika barua nyingine ya kutengua barua yake ya kujiuzulu na kutangaza kurejea rasmi katika wadhifa wake huo. Uamuzi huo ulikigawa chama na kuwa na pande ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na nyingine ikimuunga mkono Profesa Lipumba. Licha ya kambi hiyo kumpinga, Msajili wa Vyama alitangaza kumtambua Profesa Lipumba akidai mchakato wake wa kujiuzulu ulikuwa haujakamilika
Hivyo Msajili alisema kuwa licha ya kuandika barua hiyo ya kujiuzulu, lakini bado alikuwa ni mwenyekiti halali, kwani mamlaka iliyokuwa imemteua ambayo ni Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho, ilikuwa haijaridhia, kama katiba yao inavyoeleza.
Kutokana na uamuzi huo ndipo kambi ya Maalim Seif kupitia kwa baadhi ya wajumbe wa bodi waliokuwa upande wake ilifungua kesi mahakamani hapo ikidai kuwa Msajili hana mamlaka hayo kwani hayo ni masuala ya kiutawala ya ndani ya chama ambayo hawezi kuyaingilia.