- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HUKUMU YA KINA MBOWE NA WENZAKE YASOMWA
Dar es Salaam . Hukumu ya kesi inayowakabili viongozi 7 wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe imeanza kusomwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Machi 10, 2020 saa 7:00 mchana Kamili licha ya kuwepo kwa heka heka za wafuasi wa viongozi hao na polisi.
Hukumu hiyo inasomwa na Hakimu Mkazi mkuu wa Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba huku ulinzi ukiwa umeimarishwa ndani, nje ya mahakama hiyo. Hukumu hiyo inasomwa katika mahakamani ya wazi namba moja.
Idadi kubwa ya wananchi na wafuasi wa chama hicho wamezuiwa kuingia mahakamani, kutakiwa katika nje. Katika kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018 washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kati ya Februari 1 na 16, 2018. Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiwemo wabunge na wenyeviti wa kanda ni miongoni mwa waliojitokeza kusikiliza hukumu hiyo.
Wengine ni kutoka vyama vingine vya upinzani akiwemo mshauri mkuu wa ACTWazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad. Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji. Katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika; naibu katibu mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Esther Matiko (Tarime Mjini); Halima Mdee (Kawe); Ester Bulaya (Bunda) na John Heche (Tarime Vijijini)