Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:26 pm

NEWS: HUKUMU KESI YA VIGOGO CHADEMA KUTOLEWA MACHI 10

Hatimaye Hukumu dhidi ya Kesi Na.112/2018 inayowakabili Viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na baadhi ya Wabunge wake saba kutolewa Machi 10, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam majira ya Saa 4 asubuhi.(Anaandika Deyssa h. Issa)

Mawakili wa upande wa Jamhuri na wa upande wa Utetezi wamepewa siku tano kuwasilisha mawasilisho kwa maandishi (written submission) mahakamani hapo kabla ya Hukumu hiyo.

Uwamuzi huo umetolewa leo Februari 24, 2020 na Hakimu Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo.

Septemba 12, mahakama ya Kisutu iliwapata na kesi ya kujibu viongozi tisa wa ngazi ya juu wa chama hicho akiwemo mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa Freeman Mbowe na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt Vicent Mashiji ambaye amekihama chama hicho na kutimkia chama tawala CCM.

Viongozi hao Wanakabiliwa na kesi ya uhalifu , yenye makosa 13 ukiwemo uasi.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya waendeshamashtaka kukamilisha utoaji wa ushahidi wao dhidi ya washtakiwa hao.

Hakimu Simba alisema kuwa kwa kuzingatia ushahidi uliowasilishwa na mashahidi wa upande wa uendeshamashtaka na nyaraka nyingine zilizowasilishwa mahakamani anaamini kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.

Miongoni mwa mashahidi wa upande wa uendeshamashtaka katika kesi hii pamoja na mkuu wa upelelezi kutoka Wilaya ya Kipolisi ya Mbagala, Bernard Nyambari 42 ), ambaye alieleza mahakama hiyo kuwa hotuba zilizotolewa na viongozi wa Chadema katika mkutano wa kufunga kampeni ya uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni, zilizofanyika katika viwanja vya Buibui ndio chanzo cha wananchi kuandamana.

Mwaka 2018 viongozi hao waliwahi kuweka katika gereza la Segerea baada ya hakimu mkazi kuwaondolea dhamana:

Sambamba na Bwana Mbowe washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni pamoja na mbunge wa Tarime mjini , Esther Matiko; Mbunge wa iringa mjini , Peter Msigwa; Naibu Katibu mkuu- Zanzibar, Salum Mwalimu; mbunge wa Kibamba , John Mnyika; mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa Tarime vijijini , John Heche, Mbunge wa Bunda , Ester Bulaya na Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Vicent Mashinji.