Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:33 pm

NEWS: HUENDA UINGEREZA WAKAINGIA KWENYE UCHAGUZI MKUU BILA MATARAJIO

Picha inayohusiana

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameitisha kikao cha baraza la mawaziri baadae leo na huenda akawataka wabunge waunge mkono hoja ya kuitisha uchaguzi ikiwa watapiga kura ya kuipinga serikali yake kuhusu suala la Brexit.

Tokeo la picha la boris johnson

Kwa mujibu wa taarifa ya mhariri wa masuala ya siasa wa Shirika la utangazaji la BBC, pana uwezekano mkubwa mnamo wiki hii kwa Waziri mkuu Johnson kupendekeza kwa wabunge, wazo la kuitisha uchaguzi. Wakati huo huo waziri mkuu wa zamani Tony Blair amemshauri kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Jeremy Corbyn kuepuka mtego wa kufanyika uchaguzi mkuu kabla ya suala la Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya halijatatuliwa.

Bwana Blair ameeleza kwamba waziri mkuu Johnson na wanaomuunga mkono wanafanya hila ili ionekane kana kwamba chama cha upinzani, cha Labour ndicho kinachoshikilia uchaguzi wakati yeye Johnson anafanya matayarisho ya nguvu kwa ajili ya uchaguzi huo.

Waziri mkuu huyo wa zamani amekishauri chama cha Labour kipinge uchaguzi kufanyika sasa ikiwa serikali ya waziri mkuu Boris Johnson inataka kulazimisha.