Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:42 am

NEWS: HUDUMA ZA AFYA ZAWALIZA WANANCHI WA LUGALA.

DODOMA: Wananchi wa kijiji cha Lugala nje kidogo ya mji wa Dodoma wameiomba serikali kuboresha utoaji hduma bora za Afya ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ambapo kwa mujibu wa takwimu za muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama za mwaka 2015/16 zinaonyesha kila siku watoto wachanga 180 wanafariki wakati wa kuzaliwa.


Kilio hicho kimetolewa na wadau kutoka muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama pamoja na wananchi wa kijiji cha Lugala huku lengo kuu la mkutano huu wa hadhara ni kutoa elimu kwa wananchi kuona namna ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi

Wakizungumza katika mkutano huo baadhi ya wananchi wamesema kuwa ipo haja ya kuboreshwa kwa utoaji hudumza za Afya ya mama na mtoto pamoja na kuboresha miundombinu ya usafiri pamoja na kuongeza watumishi wa sekta ya Afya


Rose Mlay ni Mwenyekiti wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama anasema kuwa vifo vya mama na mtoto vimekuwa vikiongzeka hivyo kuna kila sababu ya wananchi kushirikiana na serikali na kwamba licha ya jitihada za serikali za kupunguza vifo hivyo bado vimekuwa vikitokea


Felister Charles ni muuguzi wa Zahanati ya Lugala amesema moja ya changamoto inayosababisha vifo vya mama na mtoto ni kukosekana kwa watumishi wa kutosha katika zahanati pamoja na vituo vya Afya


Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Dodoma Felister Bura amesema kuwa licha ya jitihada zinazofanywa na serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto kuna kila sababu sasa ya wananchi kushiriki katika kupunguza vifo hivyo kuanzia ngazi ya familia hadi serikali kuu


Kwa mujibu wa bajeti ya wizara ya Afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto ya mwaka 2017/18 inaonyesha kuongeza kwa bajeti katika eneo la kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa ajili ya kushughulikia huduma za dharula kutoka Bilioni 16 mwaka 2016/17 hadi kufikia bilioni 32 mwaka 2017/18