- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HOSTELI ZA CHUO CHA U-DSM ZAGEUZWA KUWA KARANTINI
Serikali imetangaza rasmi kwamba wasafiri wote kutoka nchi za nje zilizoathirika na ugonjwa wa Corona watalazimika kukaa karantini kwa muda wa siku 14 katika hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam maarufu hosteli za Magufuli.
Akizungumza katika hosteli za Magufuli, leo Aprili 5, 2020 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema wasafiri hao watafikia katika hosteli za Magufuli ambazo zipo katika eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam.
“Lengo ni kuhakikisha tunadhibiti mienendo ya wasafiri hawa.Tumeona taarifa ambazo zimetoka kule Iringa, kuna baadhi ya wasafiri tuliwaweka hotelini wakatoroka sasa ili kudhibiti mienendo ya wasafiri hawa na kuwalinda Watanzania wengi tumeona kuna ulazima wa kuwaweka sehemu moja ambako kutakuwa na ulinzi wa saa 24 na mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam,Bw. Paul Makonda atasimamia kwa karibu chini ya Wizara ya Afya,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi waelewe kwamba wasafiri hao si wagonjwa kwa sababu wanatoka kwenye nchi zenye maambukizi yenye virusi vya Corona (Covid-19) hivyo wasichukuliwe kama ni wagonjwa. “Tunawachukulia kwamba miongoni mwao kuna mmoja, wawili au watu watatu wakawa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Tutawaweka hapa kwa siku 14 kwa lengo la kuwaangalia afya zao, itakapofika siku 14, wale ambao hawajaonyesha dalili zozote tutawaruhusu waende majumbani kwao lakini wale watakaoonyesha dalili ndani ya siku tano, sita, Saba, nane hadi siku ya 14 tutachukua sampuli na kuwapima ili kujiridhisha Kama wana virusi vya Covid-19,” amesema Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa kwa mujibu wa taarifa za maabara hali ya wagonjwa waliopata maambukizi ya Covid-19 ni 20, tumepata kifo kimoja, wagonjwa watatu wamepona na wamesharudi nyumbani.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameishukuru Wizara ya Afya kwa namna ambavyo imekuwa ikipambana kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Corona nchini.