- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HOSPITALI YA MOMBASA YATEKETEA KWA MOTO
TAHARUKI imetanda usiku wa jumanne katika Hospitali binafsi ya Mombasa Hospital baada ya moto kuteketeza jengo moja la wodi ya watoto katika hospitali hiyo.
Kamishna katika Kaunti ya Mombasa Bw Gilbert Kitio akithibitisha kutokea kwa mkasa huo amesema moto huo ulianza mwendo wa saa tatu usiku katika eneo la jikoni kabla ya kusambaa.
Zimamoto kutoka kaunti hiyo wamekuwa wakifanya kulihali kujaribu kudhibiti moto huo ili usienee.
Muda wa saa moja baadaye, moto huo ulikuwa haujazimwa kabisa.
Bw Kitio ameeleza kuwa hakuna aliyejeruhiwa japo baadhi ya wagonjwa, ilibidi wahamishwe na kupelekwa hospitali jirani kwa usalama.
Walio katika eneo la mkasa ambao wamesema sehemu zilizoathirika zaidi ni chumba cha wagonjwa mahututi, wodi ya uzazi na baadhi ya wodi nyinginezo.
Jumatatu hospitali kuu ya Pwani ya Makadara palitokea moto hapo, lakini haukuwa mkubwa na ulizimwa upesi.