- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HOSPITAL YA BMH YASAINI MKATABA NA NCHI YA CUBA.
DODOMA: Hospitali ya Benjamini mkapa iliyopo jijini Dodoma umetiliana saini Mkataba wa makubaliano na Nchi ya Cuba kwaajili ya kupokea Madaktari Bingwa toka nchini Cuba lengo likiwa ni kushirikiana katika huduma ya Afya.
Akitoa taarifa kabla ya kusaini mikataba hiyo, Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk. Alphonce Chandika amesema kuwa wataalam hao ambao ni madaktari bingwa saba wataingia nchini wakati wowote na hivi sasa michakato ya kuwepo kwa inaendelea.
Dk Chandika amesema kuwa madakatari hao bingwa saba ni wabobezi katika maabara ya moyo, uchunguzi wa mfumo wa chakula na utumbo mpana, upasuaji, chumba cha wagonjwa mahututi(ICU) akiwa na muuguzi mmoja,daktari chumba cha majeruhi, mtaalam wa upasuaji wa ubongo pamoja na mtaalam wa dawa za usingizi.
"Tanzania hususan Dodoma kupitia hospitali hii tutawapata madaktari hawa wa Cuba tunajivunia matunda aliyoacha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutokana na mahusiano mazuri yaliyokuwepo baina yake na Rais wa nchini Cuba Fidero Casto, "amesema
Hata hivyo amesema kuwa hao ni madaktari ambao watakuwa wakishirikiana nao katika utoaji huduma za afya na huo ni mwanzo tu na watakapokuwa na uhitaji tena watasaini mikataba mingie.
"Kutokana na mahusiano yetu mazuri baina ya Cuba na Tanzania imesaidia pia kupunguza gharama kwani kuwachukua madaktari bingwa toka nje ya nchi ni gharama kubwa katika kuwalipa mishahara, "amesema
"Hivi sasa daktari mmoja bingwa ukimchukua nje ya nchi unamlipa mshahara sio chini ya dola 8000 kwa mwezi hivyo kwetu sisi imetusaidia sana kwani madaktari hawa wangeendq nchi nyingine wangelupwq fedha nyingi zaidi,"amesema
Kwa upande wake Balozi wa Cuba nchini Tanzania, profesa Lucas Domingo amesema kuwa anafurahia kuwepo kwa mashirikiano mazuri baina ya Tanzania na Cuba kutokana na historia ya awali baina ya nchi hizo.
Profesa huyo amesema kuwa madaktari hao wataweza kushirikiana vizuri na madaktari watanzania wa hospitali ya Benjamini Mkapa ili kuboresha sekta ya afya na afya za watanzania kwa ujumla.