- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HOJA 5 ZA ZITTO KABWE KWA MSAJILI WA VYAMA VYA KISIASA
Kiongozi mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amejibu hoja tatu za msajili wa vyama vya siasa nchini ya kutaka kukifuta chama cha chama hicho kwa madai ya kukiuka kanuni na sheria za vyama vya siasa hapa nchini.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema hoja ya Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa kudai kwamba ACT imekiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kutopeleka kwake hesabu zilizokaguliwa kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kama sheria inavyotaka amesema sio kweli "Tuhuma hizi hazina ukweli wowote. ACT Wazalendo ilianzishwa na kupewa Usajili wa Kudumu tarehe 5 Mei, 2014 na kwa hivyo, kwa mwaka huo wa fedha (2013/14) Chama chetu kilikuwa na miezi miwili tu ya kukaguliwa. kama chama cha siasa ni kuwasilisha ripoti kwa ajili ya kukaguliwa na CAG. Ripoti ya hesabu za 2013/14 imewasilishwa kwa CAG kwa barua" amesema Zitto
''Kwa kutumia Kanuni za Kimataifa za Kihasibu na kwa ushauri wa CAG, chama chetu kilielezwa kinaweza kuunganisha hesabu za mwaka 2013/2014 na 2014/2015 katika ripoti moja, wakieleza kuwa hilo jambo la kawaida kabisa katika kanuni za uhasibu kwani inaruhusiwa kuunganisha hadi miezi 18. Kwa kuunganisha huku hesabu, ACT ilikuwa na miezi 14 tu"
Akizungumza leo Machi 26, 2019 na waandishi wa Habari Makao makuu ya chama Jijini Dar es salaam Zitto amekanusha vikali chama chao kuhusika na kuchoma bendera za chama kingine "Chama chetu HAKIHUSIKI kabisa na uchomaji wa bendera wala kadi za Chama chochote. Kihistoria sisi ni Chama cha Masuala, tunaojikita juu ya Utetezi wa Wakulima wa Korosho, Mahindi, Giligilani, Karafuu, Mkonge na Mbaazi wanaokosa masoko ya bidhaa zao. Sisi tumezoeleka kuwa ni wapaza Sauti za Wafuagaji wanaotaifishiwa Mifugo yao na Wavuvi wanaonyang’anywa nyavu zao" amesema Zitto
Aidha Kiongozi huyo amejibu hoja ya msajili kwamba wanachama wao kuonekana wametumia maneno takbira kwenye shughuli za kichama na kwamba maneno hayo yana udini. amesema Majibu ya hili ni kama kwenye suala la kudaiwa kuchoma kadi na bendera. Msajili hajaainisha hao wanaodaiwa kuwa ni wanachama wetu wana kadi namba ngapi za uanachama na ni kutoka tawi gani la chama chetu.
"ACT Wazalendo ni chama cha siasa cha watu wa matabaka na dini zote na hata wale wasio na dini. Katika Katiba yetu ya chama tumeonyesha wazi kwamba hatufungamani na dini yoyote na ndiyo sababu tumeruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa.
Tuna ushauri tu kwa Ofisi ya Msajili, katika nchi ambayo Viongozi karibu wote wa Serikali wanaanza hotuba zao kwa salamu za kidini za “Bwana Yesu Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo na Assalaam Aleykum” ni rahisi kwa “wanaodaiwa kuwa wanachama wa ACT Wazalendo” kutumia kaulimbiu za Dini zao kama wanavyofanya Viongozi wa Serikali"
Barua ya Msajili haina nia njema kwa ACT Wazalendo na wapenda demokrasia wote hapa nchini. Kukosekana kwa nia njema kulionekana mapema kabisa baada ya barua iliyotakiwa kutumwa kwetu kusambazwa kwanza katika mitandao ya kijamii kabla hata haijatufikia ofisini. Taswira tunayopata ni kwamba ilivujishwa makusudi na ofisi ya msajili kutimiza dhamira ovu waliyonayo dhidi yetu.
Serikali na Chama cha CCM vimepata mchecheto na ufuasi mkubwa wa chama chetu, hasa baada ya Maalim Seif Sharif Hamad na waliokuwa Viongozi wenzake kutoka chama cha CUF kuhamia ACT Wazalendo. Wameogopa zaidi kuwa sasa ACT Wazalendo ndio kimbilio la Wazanzibari wote waliomchagua Maalim Seif kuwa Rais wao kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.
Ushauri tu kwa CCM na Serikali yake, hata wasiwaze tu kuifuta ACT Wazalendo, hatua mbaya ya namna hiyo ya kionevu itawanyima fursa karibu theluthi moja ya Watanzania ya kufanya siasa kwa njia halali za kisheria. Watu hawa wakinyimwa fursa hii kionevu kupitia ACT Wazalendo watatumia njia nyengine zinazoweza hata kuleta mpasuko kwa Taifa letu. Ikifika hatua hiyo, sisi Viongozi wa ACT Wazalendo hatutakuwa na sauti ya kuwakataza watu hawa watakaodhulumiwa fursa ya kufanya siasa kwa njia halali za kisheria.