- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HIZI NDIZO SHULE 10 BORA KITAIFA.
Dodoma: Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, na kuziorodhesha shule 10 Bora zilizofanya vyema katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.
Wakati shule binafsi zikifanya vyema, mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika mtihani huo ni wa shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, Hope Mwaibanje.
Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Januari 24, 2019 mkoani Dodoma katibu mkuu wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amezitaja shule hizo kuwa ni St Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa).
Katika matokeo hayo, watahiniwa 252 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na kati yao, 71 ni wa kujitegemea huku wawili kati yao wakiandika matusi