- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HISPANIA INAJIANDAA KUWAPATIA MAKAZI WAINGEREZA 400,000
Uhispania iinapanga kuwapa makaazi raia 400,000 kutoka Uingereza kama Uingereza itajiondoka katika Umoja wa Ulaya bila makubaliano, limeripoti gazeti la El Pais, siku moja baada ya serikali ya Uhispania kuchapisha hatua ambazo inapanga kuchukuwa.
Ili hatua hii itumike, hata hivyo, Madrid itahitaji usawa kwa wananchi wa Uhispania wanaoishi na kufanya kazi nchini Uingereza, gazeti la Al Pais limeongeza.
Kipaumbele cha Uhispania ni kwamba hakuna raia wa Uhispaniola au Uingereza atakadhulumiwa haki zake baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, Waziri wa Mambo ya Nje Josep Borrell amewambia waandishi wa habari baada ya kuhojiwa leo Ijumaa na gazeti la El Pais.
Mpango wa dharura wa Uhispania pia unahusu kesi la Gibraltar, gazeti hilo limeandika, ingawa Madrid itahitaji kuwa na kauli kuhusu hatua yoyote kuhusiana na rasi hiyo.
Rasimu ya sheria inayojumuisha hatua za mpango wa dharura itawasilishwa haraka kwa Bunge, kabla ya kufutwa kwa minajali ya uchaguzi wa haraka wabunge mwishoni mwa mwezi Aprili.