- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HIKI NDIO CHANZO CHA KIFO CHA MWENYEKITI WA CHADEMA NDESAMBURO
Kilimanjaro: Kifo cha Mwnyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa kilimanjaro Phelimon Ndesamburo Kimeleta mshtuko mkubwa sana Nchini, Ndesamburo alifariki dunia katika Hospitali ya Rufani ya KCMC mkoani Kilimanjaro jana alikopelekwa baada ya kuzidiwa ghafla akiwa ofisini kwake, katika jengo la hoteli yake ya Keys iliyoko mjini kilimanjaro.
Akitoa taarifa juu ya kifo chake Kiongozi wa jopo la madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa Ndesamburo, Prof. Elisante Massenga, "alisema jana kuwa taarifa ya awali ya uchunguzi inaonyesha kuwa kifo cha ghafla cha Ndesamburo kimetokana na matatizo ya moyo"
bila kufafanua zaidi, Prof. Massenga alisema bado walikuwa wakieendelea na uchunguzi uliokuwa ukihusisha vipimo mbalimbali na kwamba baada ya hapo ndipo watakapotoa taarifa kamili kwa wahusika.
Taarifa ya mwenyekiti wa CHADEMA freeman mbowe
Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mhe. Philemon Ndesamburo aliyefariki mapema leo Jumatano Mei 31, 2017, majira ya asubuhi. Ni huzuni kubwa na maumivu makali yasiyoelezeka kwa kumpoteza Kiongozi na Mzee watu.
Mzee Ndesamburo ni mmoja wa waasisi wa Chama Chetu cha CHADEMA na siasa za mabadiliko kwa ujumla nchini. Amekuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa miaka 15, ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro na Mjumbe Baraza Kuu la CHADEMA na juzi tu siku ya Jumamosi 27 Mei 2017 alishiriki kikao cha Baraza Kuu mjini Dodoma.
Leo alikuwa na miadi ya kukutana na Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Lazaro Kalist kwa ajili ya kumpatia rambirambi yake kwa watoto wa Shule ya msingi ya Lucky Vincent ya Arusha waliofariki katika ajali mbaya gari hivi karibuni.
Mstahiki Meya alifika ofisini kwa Mhe. Ndesamburo, ili aandikiwe hundi hiyo, wakati amechukua kalamu aandike hundi hiyo ghafla Mzee wetu akajisikia vibaya akaangua hivyo akalazimika kukimbizwa hospitalini ambapo mauti yalimkuta.
Chama kimempoteza mpambanaji na mpigania ukombozi na mabadiliko ya kweli ndani ya Taifa, alifahamu kupigania na kutafuta haki, uongozi bora na demokrasia katika Taifa letu.Kwa niaba ya chama na viongozi wenzangu, natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote bila kusahau wanachama, wapenzi wote wa CHADEMA nchi nzima na Watanzania wote walioguswa na msiba huu mkubwa kwa kumpoteza Kiongozi wetu.
Nimekuwa nikirudia kusema kila mara katika maisha ya mwanadamu huu ndio wakati mgumu kuliko wote, Mwenyezi Mungu awatie nguvu familia ya Mhe. Ndesamburo katika wakati huu mzito wa majonzi ya msiba huo tuko pamoja.
Ingawa kimwili hatuko nae lakini, hekima, busara na matendo yake yataishi milele yakifanya akumbukwe daima.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe. Amen