Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:18 am

NEWS: HECHE ATEMA CHECHE SIOGOPI KUKAMATWA

DODOMA: MBUNGE wa Tarime Vijijini Jonh Heche (Chadema) amesema kuwa yeye haogopi kuunganishwa na wananchi ambao ni wapiga kura wake waliovamia mgodi wa North Mara waliovamia mgodi huo kwa kuunga mkono juhudi za rais za kupambana na wizi na utoroshwaji wa madini.

Kauli hiyo aliita jana bungeni alipokuwa akitoa taarifa bungeni baada ya mbunge wa Viti Maalum,Jacline Msongozi (CCM) kudai Heche akamatwe na aunganishwe na waliovamia mgodi kwani yeye ndiye aliyewahamasisha.

Msongozi akichangia katika mjadala wa hotuba ya bajeti ya serikali alisema vurugu zinazoendelea kule tarime zinatokana na mbunge wao kwa kuwahamasisha kuvamia mgodi huo hivyo jeshi la polisi linatakiwa kumuunganisha mbunge huyo.

Akitoa taarifa kwa mwenyekiti wa Bunge,Mussa Zungu, Heche alisema yeye wakati akichangia alisema kuwa wananchi wanatakiwa kumuunga mkono rais katika kuzuia wezi ambao wamekuwa wakitorosha madini.

“Taarifa Mwenyekiti, napenda kumpa taarifa mchangiaji ambaye anaendelea kuchangia wananchi wa Tarime walimuona rais akiwa nahutubia akisema anazuia wezi ambao wamekuwa wakitorosha madini.

“Kutokana na hali hiyo wananchi walichukua hatua ya kumuunga mkono rais katika kuzuia wezi wa madini ambao wamekuwa wakitorosha madini lanini jeshi la polisi linatumia nguvu kubwa kuwashambulia wananchi hao.

“Hata hivyo nataka kumwambia mbunge kuwa mimi siogopi kuunganishwa na wananchi wangu kama unadhani mimi ninaogopa basi kaniunganishe wa wananchi hao” alisema Heche.

Katika hatua nyingine mbunge huyo Jacline Msongosi amejikuta akipatwa na aibu bungeni baada ya kulazimishwa kufuta kauli yake aliyoitoa jana bungeni kwa kudai kuwa wabunge wa Chadema na viongozi wa chama hicho waliokula fedha za rambirambi zilizotolewa kwenye msiba aliyekuwa mbunge mstaafu wa Moshi Mjini na Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema marehemu Philimon Ndesambulo.

Mbunge huyo akimalizia kuchangia alisema waende kule wapinzani kwa kula pesa za rambirambi za marehemu Ndesambulo.

Kutokana na kauli hiyo kaimu Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Cecilia Paresso (Chadema)alisimama na kuomba mwongozo wa kiti kwa kumtaka mbunge huyo afute kauli au athibitishe kama wapo watu waliokula fedha za marehemu Ndesambulo.

Baada ya Paresso kuomba mwongozo mwenyekiti wa Bunge Idd Azan Zungu akijibu mwongozo huo alimtaka Msongozi kufuta kauli hiyo na kama hatafanya hivyo ni vyema akathibitisha.

Msongozi alilazimika kufuta kauli aliyoitoa bungeni kuwa wapo watu wa chadema wamekula rambirambi aliyekuwa mbunge mstaafu wa Moshi Mjini na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Dk.Philimini Ndesamburo na kusema kuwa kwa sababu ni suala la msiba anafuta kauli yake.

Awali mbunge wa Tarime Vijijini John Heche alilazimika kuomba mwongozo kutokana na matukio ambayo yanaendelea kule katika ngodi wa Narth Mara.

Akiomba muongozo wa Mwenyekiti bunge, Mussa Azzani Zungu, Heche alisema “Mheshimiwa mwenyekiti kama mulivyosoma kwenye vyombo habari, jana na leo asubuhi, wananchi wa Tarime eneo la Nyamongo, wamemuunga rais mkono kwa vitendo, kwa kuingia kwenye mgodi wa North Mara kuzuia wizi ambao kamati zote za rais zimethibitisha na rais amewatangazia wananchi.

“Sasa mwenyekiti jambo la ajabu ni kwamba polisi wanatumia nguvu kubwa sana kupiga wananchi kuwaumiza, kinyume cha utaratibu wa rais alivyoagiza. Sasa mwenyekiti naomba muongozo wako,” alisema Heche wakati akiomba muongozo huo.

Hata hivyo, Jacline alisema hakuna sehemu yeyote ambayo Rais Magufuli ameagiza wananchi wavamie migodi na kwamba wanaofanya hivyo, ni wahalifu kama wahalifu wengine, hivyo alilitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua kali.

Akijibu muongozo wa Heche, Zungu alimuomba mbunge huyo kuonana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchembe, ili wapate njia muafaka wa kuweza kulitatua.