- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HAUNA KITAMBULISHO HAUINGII GESTI JOMBE
Njombe. Mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amesema watu wote wanaoingia kwenye nyumba za kulala wageni ni lazima waonyeshe kitambulisho kinachotambulika na Serikali la sivyo haupati huduma hiyo.
Msafiri ametoa kauli hiyo leo Jumamosi wakati akizungumza na maofisa ustawi wa jamii ngazi ya wilaya na kata katika semina ya Kamati ya Ulinzi wa Mwanamke na Watoto iliyokuwa ikitolewa na maofisa kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto.
Semina hiyo pia ilitoa mafunzo na namna ya kukabiliana na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto yanayoendelea wilayani Njombe.
“Katika kipindi hiki tuhakikishe tunajisimamia maeneo yetu tunayoishi. Mgeni yeyote iwe ni kijijini au mjini tutoe taarifa kwa viongozi wetu na kwenye nyumba za kulala wageni tumeshatoa maelekezo.”
“Kila anayeingia nyumba ya kulala Njombe hii awe na kitambulisho ninaamini hakuna mtu atasema hana kitambulisho cha mpiga kura au cha taifa kama huna basi wewe si raia wa Tanzania,” amesema Msafiri.
Amesema mtu ambaye hatakuwa na kitambulisho chochote kile awe na barua ya utambulisho alikotoka vinginevyo hatakubaliwa kupokelewa popote ndani ya wilaya yake.
“Tunafanya hivyo si kutaka kuwanyanyasa hapana bali ni kuona suala la ulinzi na usalama linazingatiwa na tunakuwa salama zaidi,” ameongeza.