- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HATIMAYE WANAWAKE SAUDI ARABIA WARUHUSIWA KUENDESHA MAGARI
Riyadh: Mfalme wa Saudi Arabia Salmane ametoa agizo la kuruhusu wanawake kupewa leseni bila kujali jinsia yake,
Agizo hili imekuwa ni hatua kubwa kwa wanaharakati ambao wamekua wakidai haki hii na hata kufungwa kwa kudharau marufuku iliyokuwepo awali. Agizo hili litaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Juni mwaka wa 2018 katika nchi hiyo ya Ghuba.
"Ninashtuka, ninafurahi sana," amesema Haya Rakyane, mfanyakazi wa benki mwenye umri wa miaka 30. "Sikuweza kutarajia uamuzi huo kabla ya miaka 10 au 20," aliliambia shirika la habari la AFP.
"Ni siku ya furaha sana! Sijaamini hivyo bado, Siamini kabla ya kuona kwa macho yangu mwenyewe," amesema kwa upande wake Chatha Dousri akiliambia shirika la habari la AFP.
Wanawake wengi kutoka Saudi Arabia ambao wanaweza kuendesha gari London au Dubai lakini hapana Riadh walijaribu kusisitiza kuondolewa kwa marufuku haya nchini Saudi Arabia lakini walikamatwa.
Marekani ilijibu vyema kwa uamuzi wa mshirika wake mkubwa katika ukanda wa Mashariki ya Kati kwa kuruhusu wanawake kuendesha gari, huku rais Donald Trump akisema ni "hatua chanya kwa kuendeleza haki za wanawake nchini Saudi Arabia."
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, pia amekaribisha uamuzi huo wa Saudi Arabia.