- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HATIMAYE WANANCHI WA UFARANSA WAPATA RAIS MPYA KIJANA
UFARANSA: Wapiga kura nchini Ufaransa juma pili ya jana ya tarehe 7 wamemchaguwa rais mpya Bw Emmanuel Macron Kuwa Rais wa nchi hiyo, Macron anakuwa rais kijna kwenye historia ya nchini ufaransa. Uchaguzi ulikuwa kati ya mgombea wa kujitegemea wa sera za mrengo wa kati Emmanuel Macron na kiongozi wa sera kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen katikachaguzi muhimu kwa mustakbali wa nchi hiyo na Ulaya
Macron amemshinda mwenzie bi Le pen kwa zaidi ya asilimia 65.8% ya kura zote ambapo ni sawa na kura 20,429,650, wakati Le pen alipata 10,608,109 ya kura zote sawa na asimilimia 34.2% ya kura
Uchaguzi huu unafuatia kampeni kali za kushutumiana, kashfa, mambo ya maajabu na shambulio la udukuzi la dakika za mwisho dhidi ya Macron mtaalamu wa zamani wa benki ya uwekezaji mwenye umri wa miaka 39 ambaye hakuwahi kushika madaraka kwa kuchaguliwa na wananchi.
Marine Le Pen aliyekuwa na matumaini ya kuikwaa nafasi ya rais wa Ufaransa tayari amekubali kushindwa dhidi ya mpinzani wake Emmanuel Macron.
"Watu wa Ufaransa wamemchagua rais wa Jamhuri, na wameamua kuwa na muendelezo. Nimempigia simu bwana Macron kumpongeza kutokana na ushindi wake kwasababu nina wiwa moyoni mwangu na ninaitakia mema nchi hii.