- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HATIMAYE UPINZANI CONGO WASHINDA KITI CHA URAISI
Felix Tshisekedin ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Desemba 30 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiashiria ubadilishanaji madaraka wa amani kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.
Tume ya taifa ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, CENI, imetangaza ushindi wa Tshisekedi alfajir ya leo Alhamis, na ushindi huo umekuwa wa kushtukiza kwa wengi ambao walishuku kuwa matokeo hayo yangebadilishwa ili mgombea wa muungano wa vyama tawala, Emmanuel Ramazani Shadary awe ndie mshindi. Shadary alikuwa mgombea aliyeteuliwa mahsusi na rais anayeondoka madarakani, Joseph Kabila.
Takwimu zilizotangazwa na CENI zimeeleza kuwa Tshisekedi amepata kura milioni 7, sawa na asilimia 38 ya kura zote zilizopigwa, akifuatiwa na mgombea mwingine wa upinzani, Martin Fayulu aliyeungwa mkono na watu milioni 6.3, naye Shadary wa muungano wa vyama tawala akaja katika nafasi ya 3 akiwa na kura milioni 4.3. Wagombea wengine waliambulia kura kiduchu.
Tshisekedi atoa heshima kwa Kabila
Baada ya kutangazwa mshindi, Felix Tshisekedi amesema anatoa heshima zake kwa Rais Joseph Kabila, ambaye amesema anamchukulia kama mshirika muhimu kisiasa.
Lakini, aliyekuja katika nafasi ya pili, Martin Fayulu, ameyapinga matokeo yaliyotangazwa, akisema hayana uhusiano wowote na ukweli uliokuwa katika masanduku ya kura.
Katika mahojiano na Radio ya Kimataifa ya Ufaransa, RFI, mwanasiasa huyo amewataka waangalizi wa uchaguzi kuchapisha alichokiita 'matokeo ya kweli'', akisema kilichotangazwa na CENI ni mapinduzi kupitia uchaguzi. Mapema wiki hii, Fayulu alikuwa amesema kuwa ikiwa tume itatangaza matokeo tofauti na waliyo nayo, yumkini akimaanisha yanayompa yeye ushindi, muungano unaomuunga mkono ungetangaza matokeo yake wenyewe, ambayo alidai yasingekuwa na mjadala wowote.