Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:20 pm

NEWS: HATIMAYE TANZANIA YAPATA JAJI MKUU MPYA

Dar es salaam: Rais Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemteua Jaji Prof. Ibrahim Hamisi Juma kuwa Jaji mkuu wa Tanzania, Prof. Juma awali alikuwa Makamu Jaji mkuu kabla ya kushika wadhifa huo.

Prof. Juma amechukuwa nafasi hiyo baada ya kustaafu kwa Jaji Mohamed Chade Othumani, Jaji Juma anashika nafasi hiyo baada ya Tanzania kukaa kwa kipindi cha muda wa Takribani miaka miwili pasi kuwa na Jaji mkuu, kumekuwepo nasintofahamu kutoka mashirika ya Raia, Tume ýa haki za minaadamu na utawala bora na Chama cha mawakili Tanzania TLS kupitia Rais wake Tundu Lissu kuhoji kwanini Rais Magufuli Hamteui Jaji mkuu Tangu kuingia kwake Mdarakani.

Awali kipindi cha Uchaguzi wa TLS Rais Magufuli aliwahi kutàmka Hadharani kuwa hawezi kumteua kamwe Jaji mkuu anaye tokana na makando kando ya kisiasa. Jaji mkuu huyo mpya anakibarua kigumu kulingana na hali ya kisiasa kwa sasa nchini Tanzania na africa mashariki kwa ujumla wake, kwa sababu watu wengi baada ya uchaguzi wa kenya uliofanyika tarehe 8 mwezi nane mwaka huu kuwa na mgogoro mkubwa wa kiasiasa hasa pale ambapo maada ya tume ya uchaguzi nchini kenya kumtangaza Rais Uhuru kenyatta kuwa Mshindi wa katika nafasi ya urais na Odinga kuupinga ushindi huo kwa kwenda mahakamani (supreme court), na Majaji 7 wa mahakama hiyo kubatilisha ushindi huo, imeonesha kuwa mahakama nchini kenya zipo huru sasa je inawezekana kwa nchi kama Tanzania.?