Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:30 pm

NEWS: HATIMAYE RAIS KABILA AKUBALI KUFANYIKA UCHAGUZI NCHINI CONGO

New york: Raisi wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amesema kuwa taifa lake linaelekea katika uchaguzi huku akiweka msisitizo kupinga mashinikizo ya kigeni katika kuandaa tarehe ya uchaguzi huo wa kihistoria.

Akihutubia katika mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Marekani Kabila ametoa wito kwa marafiki wa DRC kumuunga mkono katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kiusalama wakati taifa hilo linapoandaa uchaguzi mkuu.

Kabila alikutana na raisi wa umoja wa Afrika Alpha Conde, waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel,mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda na kamishna mkuu wa haki za binadamu Zeid Al Hussein.

Chini ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali na makundi ya upinzani mwaka jana uchaguzi unapaswa kufanyika mwaka huu katika taifa hilo na kupisha makabidhiano ya madaraka kwa njia ya demokrasia.