- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HATIMAYE NA MAREKANI YASITISHA SAFARI ZA NDEGE YA BOING 737 MAX 8
Kinachowezwe kusemwa ni kwamba hakuna namna nyingine hii ni baada ya Marekani pia kuungana na nchi zingine duniani kuamuru kusitisha safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 na MAX 9 ambayo kimsingi ni kampuni iliyopo nchini humo.
Hatua hiyo ya Marekena imechukuliwa Jumatano, Machi 13, inatafsiririwa kuwa hii ni baada ya nchi nyingi barani Ulaya kusitisha safari za ndege aina ya Boeing 737 MAX.
Juzi Jumapili Machi 10, 2019 ajali ya ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 ya shirika la Ethiopia la Ethiopian Airlines iliua watu wapatao 157 kutoka mataifa 35 jijini Addis Ababa.
Ni ajali ya pili kuwahi kushuhudiwa ya ndege hiyo chapa Max 8 katika miezi mitano baada ya ajali nyingine nchini Indonesia mwaka jana Oktoba iliosababisha vifo vya watu wengi.
Kampuni ya Boeing Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia imesitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo baada ya wachunguzi kubaini ushahidi mpya katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines ilianguka.
Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Marekani (FAA), imesema ushahidi mpya pamoja na data mpya za satelaiti zimechangia uamuzi huo wa kupiga marufuku kwa muda usafiri wa ndege hizo.
Awali rais Donald Trump alitangaza kwamba shirika la FAA litatoa tangazo la dharura kufuatia "taarifa mpya na ushahidi "kutoka eneo la mkasa na kutoka maeneo mengine kupitia malalamiko mengine tofauti'.