Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 11:19 pm

NEWS: HATIMAYE LIPUMBA ATEULIWA TENA KUGOMBE UWENYEKITI

Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Mwenyekiti anayetambulika na ofisi ya Msajili wa vyama vya kisiasa Prof. Lipumba limewapitisha wanachama watatu wa chama hicho akiwamo mwenyekiti wa sasa Profesa Ibrahim Lipumba kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho.

Kwamujibu wa Prof. Lipumba huu ni mkutano wa saba wa chama hicho uliofanyika leo Jumatano Machi 13, 2019

Pamoja na Profesa Lipumba wengine kwenye kinyang’anyiro hicho ni Diana Daudi Simba na Zuberi Mwinyi Hamisi. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe 798.

Prof. Lipumba amesema kwa sababu ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti hawezi kuwa mwenyekiti wa kikao hicho.

Amesema kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu za chama hicho kikao kipendekeze mwenyekiti wa muda.

Aliwauliza wanachama kwa ujumla wao wanamtaka nani awe mwenyekiti wa muda wakajibu. ‘Milambo Yusuph Kamili’ hivyo akamtangaza kuwa ndiyo mwenyekiti wa muda wa kikao hicho.

Awali, Profesa Lipumba ametoa ufafanuzi wa uchaguzi utakavyofanyika kuwa wataanza na kumchagua mwenyekiti wa taifa, akifuatia makamu mwenyekiti Zanzibar na kumalizia na makamu mwenyekiti Tanzania Bara.

Naye Mkurugenzi wa habari wa CUF, Abdul Kambaya amesema kinachoendelea sasa hivi ni kuchagua wajumbe watakaoshiriki uchaguzi huo.


Kambaya amesema hali ya leo katika mkutano huo itakuwa nzuri tofauti na ilivyokuwa jana. Pia amesema kutakuwepo na ulinzi wa askari ambao watakuwa wamevaa nguo za kiraia ili kuhakikisha hali ya usalama inakuwapo