- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HAMASA YA KAMPENI YA USAFI IMEZIDI KUONGEZEKA MPWAPWA.
MPWAPWA: Takribani watu 300 wameshiriki Kampeni ya Siku ya Usafi ambayo imeonyesha mafanikio makubwa katika wilaya ya Mpwapwa.
Watu hao ni pamoja na wataalamu, wakuu wa Taasisi, Wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kampeni hiyo inayolenga kuuweka mji katika mazingira ya usafi na kuondokana na magonjwa ya mlipuko imekuwa na ongezeko na mwamko mkubwa zaidi wa watu kushiriki.
Zoezi la usafi limefanyika kwenye mji mzima ikiwemo kwenye makazi ya watu Mpwapwa Mjini, Mazae, Ving'awe, Hospitali ya Wilaya na kwenye korongo kubwa la Mpwapwa pamoja na Soko Kuu na Stendi ya Mabasi
Akizungumza wakati wa zoezi hilo mkazi mmoja wa Mpwapwa Orbert Mwalyego amesema zoezi limeenda vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki.
"Tunakushukuru na kukupongeza Mhe Mkuu wa Wilaya yetu kwa support yako, siku zote umekuwa mstari wa mbele kutuonyesha njia hivyo tunakuahidi kuwa nawe bega kwa bega, "alisema mkazi huyo.